25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Neymar aipa Brazil ubingwa wa Olimpiki

1471746507_brazil-neymar-gabriel-jesus-barbosa-gold-medal-rio-olympics

RIO DE JANEIRO, BRAZIL

NAHODHA wa timu ya taifa ya Brazil, Neymar de Santos, amefanikiwa kuipa ubingwa timu hiyo katika michuano ya Olimpiki ambayo imemalizika jana nchini humo.

Brazil imetwaa ubingwa huo baada ya kuifunga Ujerumani katika mchezo huo wa fainali kwa jumla ya mabao 5-4 ya mikwaju ya penalti.

Brazil walikuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 27 kwa mpira wa adhabu, ambao ulipigwa na mshambuliaji huyo hatari na kuzama moja kwa moja wavuni. Hata hivyo, kipindi cha pili wapinzani walibadilika na kufanikiwa kupata bao la kusawazisha.

Hivyo hadi dakika 90 zinamalizika timu hizo zilikuwa sare ya 1-1, hivyo kwenye mikwaju ya penalti Brazil ilifanikiwa kushinda yote mitano, huku Ujerumani ikipoteza mkwaju mmoja.

Mkwaju wa mwisho wa Brazil ulipigwa na nahodha huyo na kuwainua mashabiki wa taifa hilo ambao walijitokeza uwanjani hapo.

Hata hivyo, mchezaji huyo alishindwa kuzuia hisia zake baada ya kuipatia ubingwa timu hiyo na kujikuta akitokwa na machozi yenye furaha kubwa.

Brazil imeonekana kulipa kisasi cha mwaka 2014 kwenye michuano ya Kombe la Dunia ambayo ilipigwa nchini humo na kujikuta wakiyaaga mashindano katika hatua ya nusu fainali, baada ya kuchezea kichapo cha mabao 7-1 dhidi ya timu ya Taifa ya Ujerumani.

Hata hivyo, katika mchezo huo wa nusu fainali ambapo Brazil ilipokea kichapo hicho, Neymar alikuwa majeruhi baada ya kuumizwa uti wa mgongo, wakati huo beki wao wa kati, Thiago Silver akiwa nje ya uwanja kwa kutumikia kadi nyekundu.

Safari hii Neymar ameonekana kuwa na mchango mkubwa katika michuano hiyo, japokuwa anadaiwa kuwa na utovu wa nidhamu.

Hata hivyo, mashabiki wa timu hiyo walianza kuizomea timu yao katika michezo miwili ya mwanzo kutokana na matokeo mabaya ambayo waliyapata, hasa katika mchezo wa kwanza dhidi ya Afrika Kusini ambapo ulimalizika kwa suluhu pamoja na mchezo dhidi ya Iraq katika hatua ya makundi.

Baada ya hapo walionekana kuwa na mshikamano na kuanza kuwachapa wapinzani wao kwa ushindi wa mabao mengi hadi kufanikiwa kuingia hatua ya fainali.

Nyota wa zamani wa timu ya Taifa ya Brazil, Edson Pele, amewapongeza wachezaji kwa kile ambacho wamekifanya na kufanikiwa kutwaa ubingwa wa Olimpiki.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles