29.4 C
Dar es Salaam
Sunday, October 13, 2024

Contact us: [email protected]

Ibrahimovic: United itachukua ubingwa wa ligi

Zlatan Ibrahimovic
Zlatan Ibrahimovic

MANCHESTER, ENGLAND

MSHAMBULIAJI mpya wa klabu ya Manchester United, Zlatan Ibrahimovic, amedai kwamba klabu hiyo lazima ichukue ubingwa msimu huu wa Ligi Kuu nchini England.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34, hadi sasa amefanikiwa kufunga mabao matatu katika michezo miwili ambayo amecheza ya Ligi Kuu, hivyo anaamini kutokana na ubora wa wachezaji wa timu hiyo na kocha wao Jose Mourinho, kuna uwezekano mkubwa wa kutwaa ubingwa msimu huu.

Mara ya mwisho Manchester United kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ilikuwa msimu wa 2012-13, huku timu hiyo ikiwa chini ya kocha Sir Alex Ferguson, lakini hadi sasa wamepita makocha wawili bila kuchukua taji hilo.

Ibrahimovic amejiunga na klabu hiyo ya Old Trafford katika kipindi hiki cha majira ya joto akitokea klabu ya Paris Saint-Germain ya nchini Ufaransa, na ameonesha ubora wake kwa kufunga mabao matatu katika michezo miwili ya awali ya Ligi Kuu.

“Ninaamini kwamba lazima klabu hii ichukue ubingwa, nina mtazamo huo, lakini tunatakiwa kujituma kwa hali na mali ili kuhakikisha tunatimiza malengo yetu.

“Tutahakikisha tunapambana na klabu zote ambazo zimejiandaa kwa ajili ya kutaka ubingwa msimu huu, ninachokiangalia kwa sasa ni jinsi gani ya kuisaidia timu yangu kufanya vizuri katika kila mchezo.

“Nina furaha kubwa ya kuwa na mabao matatu hadi sasa katika michezo miwili, lakini bado nina nafasi ya kuendelea kufunga kwa kuwa msimu ndio umeanza, bado nina safari kubwa ya kuendelea kufanya vizuri,” alisema Ibrahimovic

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles