23.3 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Serengeti Boys yachapa ‘Wasauzi’ 2-0

Wachezaji wa timu ya Taifa ya VIijana wenye miaka 17, Serengeti Boys, wakishangilia bao la pili lilifungwa na mshambuliaji wa timu hiyo Muhsin Makame, dhidi ya timu ya Ama Jimbos ya Afrika Kusini, katika mchezo wa marudiano wa raundi ya pili ya kuwania kufuzu  fainali za Mataifa ya Afrika kwa vijana 2017 mchezo ulichezwa katika Uwanja wa Chamanzi Dar es Salaam jana.
Wachezaji wa timu ya Taifa ya VIijana wenye miaka 17, Serengeti Boys, wakishangilia bao la pili lilifungwa na mshambuliaji wa timu hiyo Muhsin Makame, dhidi ya timu ya Ama Jimbos ya Afrika Kusini, katika mchezo wa marudiano wa raundi ya pili ya kuwania kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika kwa vijana 2017 mchezo ulichezwa katika Uwanja wa Chamanzi Dar es Salaam jana.

* Sasa kukutana na Congo-Brazaville au Namibia

Na THERESIA GASPER-DAR ES SALAAM

TIMU ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ‘Serengeti Boys’, baada ya kuisukuma nje timu ya vijana ya Afrika Kusini kwa kuifunga bao 2-0 jana, sasa inatarajia kukutana na timu kati ya Congo-Brazavile au Namibia kwenye mchezo wa mwisho wa kufuzu kucheza Fainali za Mataifa  ya Afrika 2017 kwa vijana nchini Madagascar.

Serengeti ilipata ushindi huo baada ya mchezo wa awali kuwa na matokeo ya sare ya 1-1, uliochezwa nchini Afrika Kusini kabla ya jana kuinyuka mabao 2-0 katika mchezo wa marudio uliochezwa Uwanja wa Azam Chamanzi, Dar es Salaam, hivyo kuiondoa kwa jumla ya mabao 3-1.

Matokeo hayo yatawafanya vijana hao ambao ni wawakilishi pekee wenye kuleta faraja kwa Watanzania, kucheza kufa au kupona katika mchezo wa mwisho utakaoamua kucheza fainali hizo mwakani.

Mchezo wa jana ulianza kwa kasi, huku timu zote zikisaka bao, hivyo kufanya  safu za ushambuliaji za timu hizo kuwa makini na kuhaha mara kwa mara langoni mwa timu pinzani.

Serengeti ndio waliokuwa wa kwanza kuandika bao katika dakika ya 35 kipindi cha kwanza cha mchezo, kupitia kwa mshambuliaji, Mohamed Abdallah,  baada ya kupokea krosi safi ya Hassan Juma.

Dakika ya 45 kabla ya mwamuzi wa mchezo huo, Noiret Jim Bacari, kutoka nchini Comoro kupuliza kipyenga cha mapumziko, Serengeti walipata pigo kwa mchezaji wao, Hamis Ali, kutolewa nje kwa kadi nyekundu kwa kumchezea rafu Bonga Thembelani.

Kipindi cha pili kilianza kwa Dickson Nickson kupewa kadi ya njano dakika ya 77, baada ya kumchezea rafu Jaqueel Joseph.

Hata hivyo, dakika ya 84, Muhsin Makame aliweza kuisaidia timu yake kupata bao la pili baada ya kumalizia pasi safi kutoka kwa Mohamed Rashid.

Timu hizo zilimaliza dakika 90 kwa Serengeti kuibuka na ushindi wa mabao 2-0, na hivyo kuendelea kuwa timu tegemeo kwa Watanzania.

Serengeti: Ally Hussein,  Ramadhani Kabwili, Nickson Clement Kabange, Dickson Nickson, Israel  Patrick, Ally Hamis Ngazi, Kelvin Nashona, Shaban Zubeir, Mohamed Rashid, Yohana Oscar na Asad Ally/Issa Abdi.

Afrika Kusini: Luke Gareth, Glen Tumelo, Luke Donn, Mswati Lukhele, James Thabiso, Jaqueel Joseph, Kwenzokuhle Shinga, Siphamandla Andisa, Mjabulise Mkhize, Linamandla Mchilizeli/Tyreese Pillay, Ndamolelo Radzilane/Bonga Thembelani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles