29.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 28, 2021

Ndugai ataka usawa miradi ya maji nchini

Na RAMADHAN HASSAN-DODOMA

SPIKA wa Bunge, Job Ndugai ameitaka Wizara ya Maji kuweka usawa katika ugawaji wa miradi ya maji kwani kuna maeneo wanapendelewa.

Akizungumza jana wakati wa mjadala wa bajeti ya Wizara ya Maji kwa mwaka 2020/21, Spika Ndugai alisema kwa sasa hakuna usawa katika ugawaji wa miradi ya maji kwani kuna maeneo wanapendelewa.

Alisema haiwezekani maeneo mengine vijiji viwe vichache huku mengine wakipatatiwa mamilioni ya fedha.

“Profesa tunakupitishia bajeti yako, lakini mambo ovyo, hakuna usawa, wengine kijiji kimoja wengine wanapata mamilioni, nasema hapana, hili linatakiwa kuangaliwa.

“Ni tatizo kubwa, unaweza ukaona wewe unapata ugali unashiba, lakini hili ni tatizo kubwa,” alisema Spika Ndugai.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
158,609FollowersFollow
519,000SubscribersSubscribe

Latest Articles