22.6 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 28, 2021

IGP Sirro atoa agizo kwa makamanda wa polisi

Na MALIMA LUBASHA-MUSOMA

MKUU wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro,  amewataka makanda wa polisi wa mikoa yote ya Kanda ya Ziwa Victoria kuhakikisha wanawatia mbaroni watakaobainika kukiuka maagizo ya Serikali na wafikishwe mahakamani kujibu makosa yao.

Agizo hilo alilitoa jana mjini Musoma, alipokuwa akizungumza na makamanda hao wa mikoa ya Kanda ya Ziwa, ambapo pia alipokea taarifa kuhusu oparesheni iliyofanyika kuhusu mauaji ya vikongwe pamoja na matukio mengine ya uhalifu zoezi ambalo pia litafanyika mikoa mingine.

Alisema kuwa suala la mipaka, jeshi hilo limejiimarisha na kutoa maagizo kwa viongozi wa vijiji kuwatolea taarifa wageni wote wanaoingia nchini ili waweze kutambuliwa.

Lengo la ziara hiyo ilikuwa ni kutoa taarifa kuhusiana na oparesheni iliyokuwa ikifanyika kanda ya ziwa kuhusiana na mauaji ya vikongwe.

Katika taarifa hiyo ilielezwa kuwa zaidi ya watu 712 waliokuwa wakihusishwa na matukio ya mauaji, wizi wa mifugo, wapiga ramli chonganishi wamekamatwa na wengine wamefikishwa mahakamani.

IGP Sirro alisema kuwa tathmini iliyofanyika kuhusu oparesheni hiyo, imeonyesha mafanikio makubwa ikifanikiwa kuwakamata watu waliokuwa wanashiriki mauaji ya ushirikina na matukio mengine ya uhalifu katika mikoa hiyo ambayo ni Tarime/Rorya, Mara Simiyu, Mwanza, Geita na Kagera.

Akizungumzia watu wanaotumia mitandao ya kijamii vibaya, amewaagiza makamanda hao kuwakamata na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria kwani wana nia ovu kwenye matumizi ya mitandao hiyo ikiwamo kutoa taarifa na takwimu za Covid -19 ambazo si sahihi na zenye lengo la kuwatia hofu wananchi.

Aaliwataka makamanda wa polisi kuhakikisha wanasimamia hatua zote za tahadhari kwa jeshi hilo iliwamo kuhakikisha askari wananawa mikono kwa sabuni na maji tiririka, kuepuka msongamano, kuvaa barakoa, kusimama mita mbili na mwenzako, kusalimiana kwa kutoshikana mikono ama kutumia vitakasa mikono.

“Ni lazima tu tuzingatie maelekezo yote yanayotolewa na wataalamu wa afya ambapo jeshi hilo limepokea vipima joto 29 vitagawanywa vituo vikuu vyote vya polisi,” alisema IGP Sirro.

Alisema kuwa mpaka wa nchi kwa sehemu kubwa uko wazi, watu kutoka nchi jirani wanavuka mpaka na wanaingia kuja kutafuta chakula, matibabu na mahitaji mengine hali inayochangia wananchi kupata maambukizi ya corona.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
158,502FollowersFollow
519,000SubscribersSubscribe

Latest Articles