25.5 C
Dar es Salaam
Thursday, September 28, 2023

Contact us: [email protected]

Ndizi tiba maridhawa kwa chunusi

banana_3546034b

Na MWANDISHI WETU,

TOFAUTI na matunda mengine, ndizi zinafaida kubwa katika mwili wa binadamu. Kwa mujibu wa wataalamu wa lishe, ndizi zina virutubisho vya aina mbalimbali kama vile, protini, mafuta, kalshiamu, wanga, fosiforas, madini ya chuma, vitamin A,B,C na maji.

Ndizi zina uwezo wa kumeng’enywa kwa urahisi zaidi, tena zina nishati, sukari iliyomo ndani yake ni chanzo kizuri cha nishati.
Husaidia kuondoa chunusi. Kwa kuchanganya ndizi mbivu, maziwa na asali na kuzisaga ili kupata urojo ambao utatumia kupaka kwenye maeneo yaliyoathirika, unaweza kuondokana kabisa na tatizo hilo.

Fanya hivyo kila siku na hakikisha unakaa na mchanganyiko huo kwa muda usiopungua dakika 30 hadi 40, kisha osha na maji ya baridi ikiwezekana yaliyopozwa na jokofu.

Ndizi katika ‘diet’ zina nafasi kubwa katika kuongeza au kupunguza uzito, hivyo unaweza kutumia ikiwa unahitaji kupunguza ama kuongeza uzito wako.
Kwa wajawazito ni chakula kizuri mno, kwani kina kiwango kikubwa cha ‘folic acid’ ambayo inaweza kufyonzwa kwa urahisi na kiumbe kilicho tumboni. Ikiwa mjamzito atatumia ndizi mara kwa mara ni wazi kuwa atakuwa mwenye muonekano mzuri na wa kuvutia.

Pia ni kinga dhidi ya magonjwa ya moyo, presha, vidonda vya tumbo, saratani ya figo na kukosa choo.

Ndizi mbivu ni tunda ambalo linafahamika na kila mtu, lakini sina hakika kama watu wengi wanafahamu umuhimu na faida za tunda hili ambalo linapatikana kirahisi sana nchini. Bei yake ni kati ya shilingi 50 na 150 tu, kiwango cha pesa ambacho kila mtu anaweza kukimudu.

Iwapo ulikuwa hujui umuhimu wa kula ndizi mbivu, leo utalazimika kubadili mtizamo wako na kuziangalia ndizi kama tunda muhimu katika kuupa nguvu na kuulinda mwili wako dhidi ya maradhi hatari ambayo hayana tiba.

Wanamichezo pia wanapaswa kuliona tunda hili kuwa ni muhimu katika kuipa miili yao nguvu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,750FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles