23.7 C
Dar es Salaam
Saturday, September 23, 2023

Contact us: [email protected]

Bila Cholestro huwezi kuwa na uhai – 4

sumber-karbohidrat

TUMESOMA vyakula vinavyoongeza TGA, LDL na kupunguza HLD, tumeona ni wanga na sukari. Sasa kwa nini unakula vyakula ambavyo vyote vinachochea?

Hapo awali tuliamini kwamba mama ambaye ananyonyesha asipopata maziwa akinywa maziwa ya ng’ombe atapona.

Lakini sayansi ya sasa inatuambia hakuna mahusiano ya kunywa maziwa ya ng’ombe na kutengeneza kwa maziwa ya mama.

Hivyo po siku tutakuja kuamini mafuta hayarundiki mafuta na hivyo ni rafiki yetu.

Moja ya historia ambayo utajifunza, mwaka 1846 alitokea mwanasayansi maarufu sana hapa duniani aliyejulikana kama Profesa Ignaz Semmelweis.

Alikuwa ni profesa wa John Hopkins School Of Public Health, alifanya utafiti katika wodi ya wanawake wanaojifungua katika hospitali ya Viena General akiangalia maambukizi yanayowapata wanawake wanaojifungua katika mazingira machafu kitaalamu “Pueperal sepsis” au yeye alipenda kutumia jina la Childbed fever.

Alihitimisha utafiti wake kwa kushangazwa na vifo vya akina mama mara tu baada ya kujifungua, kwa homa kali na maambukizi makali.

Akatoa maoni kwamba usafi lazima uzingatiwe na lazima mgonjwa azalishwe na mkunga aliyenawa mikono kwa taratibu maalumu (Hand washing technique before any aseptic procedures).

Hapa ndipo wakunga na madaktari walivyo mchukia na kutengeneza uhasama naye kwani utafiti wake ulionekana kama unawachongea madaktari na wakunga kwamba ndio chanzo cha vifo vya wakina mama wanaojifungua mazingira machafu.

Walimchukua na kumpeleka sehemu za mateso (Tunajua wengi ukikosea kama ulikuwa unafanya kazi mjini unapelekwa kijijini), yeye alipelekwa kambi ya vichaa na huko alipata mateso ya kila aina na hatimaye alifariki.

Ukweli mwishowe ulikuja kukubaliwa baada ya kifo chake.

Hadi leo hii huwezi kumzalisha mjamzito bila kuwa katika hali ya usafi ili kuepuka kumwambukiza mama magonjwa.

Huwezi kufanya upasuaji bila kunawa mikono. Profesa elimu yake tunaenzi hadi leo ingawa alifariki kwa kusimamia ukweli.

Unajifunza nini?

Kuna Pofesa na watalaamu maarufu wamepaza sauti mara nyingi kwamba “Mafuta si adui yetu bali wanga na sukari ndio adui” na jamii imepuuzia cha kushangaza bado wanauguzwa na elimu wanayong’ang’ania.

Ukiona ‘low fat’ maana yake pia ‘High sugar’ avoid not safe for you!

JARIBIO

Pima kipimo kinaitwa lipidi profile test kisha fanya hesabu hii:

CVD RISK: TGA/HDL
Ukipata jibu chini ya 3.5 uko salama. Kiafya ukipata jibu 7.3 na zaidi punguza wanga na sukari, upe mwili wako mafuta kama chanzo cha nguvu na nishati na baada ya miezi mitatu pima tena.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,701FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles