30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

NDC lawaita wawekezaji nishati mbadala

Na Nora Damian, Mtanzania Digital

Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) limewaalika wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi kuja kuwekeza katika miradi ya kuzalisha umeme kwa kutumia vyanzo mbadala kama vya upepo na jua ili kuongeza upatikanaji wa nishati hiyo nchini.

Shirika hilo lina miradi saba katika Mikoa ya Arusha, Dodoma, Iringa, Singida na Morogoro ambayo ikitekelezwa itazalisha megawati 1,426.

Akizungumza leo Machi 27,2024 na ujumbe wa wawekezaji kutoka Jimbo la Changzhou China, Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji, Sempheo Manongi, amesema maeneo yapo na miradi imeshaandaliwa hivyo wanatoa fursa kwa wawekezaji kuja kuwekeza.

Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji, Sempheo Manongi, akizungumza na ujumbe wa wawekezaji kutoka Jimbo la Changzhou China waliotembelea Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC).

“Tunauhitaji umeme kwa wingi kwahiyo kama tutapata uwekezaji katika masuala yanayohusina na ‘renewable energy’ kikubwa kwanza ni kupata utaalam wa hiyo sekta ndiyo tunachokihitaji kwa wingi.

“Uwekezaji ukitokea tutaongeza kiwango cha umeme kwenye nchi yetu kwahiyo uzalishaji wa umeme utaongezeka na hatimaye uwekezaji utazaa matunda kwa sababu ajira zitaongezeka, matumizi ya umeme usio rafiki yatapungua na kusaidia kutunza mazingira zaidi katika nchi yetu,” amesema Manongi.

Kuhusu ujumbe wa wafanyabiashara hao amesema umelanga kuja kuangalia baadhi ya maeneo ambayo wanaweza kushirikiana na kuwekeza.

“Tanzania na China ina historia inatubeba kutokana na maisha na uzoefu tuliokuwa nao kati ya serikali na viongozi waliotangulia, Jimbo la Changzhou lina maendeleo makubwa katika masuala ya viwanda vinavyotumia teknolojia ya hali ya juu hivyo utaalam na uzoefu wao katika sekta ya uzalishaji kwa ajili ya uwekezaji ndio umetusaidia kuona fursa zilizopo kati yetu,” amesema Manongi.

Ameyataja maeneo ambayo wafanyabiashara hao wameonyesha nia ya kuwekeza ni pamoja na kujenga viwanda vya kutengeneza power tillers, viwanda vya matrekta, genereta, pampu za maji, vifaa tiba na bidhaa za umeme.

Katika majadiliano hayo NDC pia imeonyesha fursa zilizopo nchini ambazo wafanyabiashara hao wanaweza kuwekeza ili nchi iweze kunufaika kwa kupata uwekezaji, ajira na kuongeza Pato la Taifa.

Maeneo hayo ni yale ya mnyonyoro wa thamani katika sekta ya kilimo, uzalishaji wa madini ya viwandani kama vile chuma na kituo maalumu cha masuala ya nishati mbadala.

“Tumewaonyesha fursa zilizopo za viwanda, maeneo ya uwekezaji katika sekta zote muhimu kwa nchi zetu ili tuweze kusisimua na kuimarisha uchumi wa nchi yetu kulingana na mahusiano ya nchi zetu,” amesema.

Amesema wanaweza kuwekeza moja kwa moja au kwa ubia kwa kuleta teknolojia hasa katika masuala ya nishati na kutoa ushauri wa kina katika maeneo hayo.

Naye Injinia Anna Nyangasi kutoka Kampuni ya Conopus inayojihusisha na uuzaji zana za kilimo na iliyoratibu ziara ya ujumbe wa wafanyabiashara hao, amesema wafanyabishara hao wanakusudia kuwekeza katika eneo la kilimo, afya, vifaa vya ujenzi na vifaa vya uchakataji.

Amefafanua kuwa katika mashine za kilimo watawekeza Dola milioni 24.5, vifaa tiba (Dola milioni 6), vifaa vya umeme (Dola milioni 2), vifaa vya ujenzi (Dola milioni 11.3) na vifaa vya uchakataji mafuta (Dola milioni 43).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles