27.6 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

ACB kuendelea kuboresha huduma kukidhi matarajio ya wateja

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Benki ya Biashara ya Akiba (ACB) imesema inaendelea kuboresha na kupanua wigo wa huduma zake ili kuendana na soko kwa lengo la kukidhi matarajio ya wateja wake.

Hayo yamesema Machi 25,2024 Mkurugenzi Mtendaji wa ACB, Silvest Arumasi, wakati wa hafla ya futari kwa wafanyakazi, wateja na wadau mbalimbali wa benki hiyo iliyofanyika Dar es Salaam.

Amewaomba wateja na umma kwa ujumla kuendelea kuiamini benki hiyo ambayo imeweza kuwahudumia Watanzania wengi na kuleta maendeleo makubwa kwa wajasiriamali na jamii nzima.

“Akiba Commercial Bank inatambua na kuheshimu imani za wateja, wafanyakazi na wadau wake na kuupa umuhimu wa kipekee katika mwezi Mtukufu wa Ramadhan,” amesema Arumasi.

Amewapongeza Waislamu wote kwa mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhan na kuwashukuru wadau wote kwa kutenga muda na kujumuika pamoja katika futari hiyo kwani kwa kitendo hicho kimeleta faraja na heshima kubwa kwao.

Amesema ACB imekuwa na utamaduni wa kufanya hafla ya kufuturisha kila mwaka kwa ajili ya kuunga mkono Waislam katika funga yao na kuboresha mahusiano ya benki na wateja.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles