24 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Ndayishimiye aapishwa kuwa Rais wa Burundi

BUJUMBURA, Burundi

HATIMAYE Burundi imemuapisha, Evariste Ndayishimiye kuwa rais wake.

Rais Ndayishimiye aliapishwa jana  mbele ya  maelfu ya wananchi wa taifa hilo na baadhi ya viongozi kutoka mataifa tofauti.

Katika kiapo chake, aliapa kulinda Katiba ya Burundi, kuheshimu umoja wa raia wa taifa hilo, kutoa haki kwa wote mbali na kutetea mipaka ya taifa hilo.

Kiapo hicho kinatokana na kifungu cha 107 cha Katiba ya nchi hiyo.

Sherehe hizo ziliofanyika Uuwanja wa michezo wa Ingoma mkoani Gitega, wakati ambapo taifa hilo limeathirika na mlipuko wa virusi vya ugonjwa wa corona.

Rais Ndayishimiye baada ya kumaliza kula kiapo, alikagua gwaride la kijeshi na baadaye kutoa hotuba .

 Muda mchache kabla ya kula kiapo,  aliombewa na baadhi ya maaskofu ambao walimtaka kufungua milango ya uhusiano mwema na mataifa mengine.

Mbali na  baadhi ya wageni hawakuvalia barakoa, raia wengi waliohudhuria hafla hiyo hawakuvaa kifaa hicho cha kuwalinda dhidi ya corona.

Hata hivyo, Shirika la Msalaba Mwekundu, liliandaa maji na sabuni kwa raia wote waliokuwa wakiingia uwanjani kuosha mikono yao.

Maelfu ya raia wa Burundi walifurika uwanjani kusubiri kuapishwa kwa rais huyo kufuatia kifo cha aliyekuwa rais wa taifa hilo, Pierre Nkurunziza.

Evariste atachukua nafasi ya Rais Nkurunziza mbaye ameliongoza taifa hilo la Afrika Mashariki kwa miaka 15.

Alizaliwa mwaka wa 1968 katika Mkoa wa Gitega, eneo la kati mwa taifa hilo.

Ni miongoni mwa waliokuwa waasi wa CNDD-FDD, waliojiunga na kundi hilo baada ya kunusurika mauaji ya kikabila ya wanafunzi Wahutu katika Chuo kikuu cha Burundi mwaka 1995, kufuatia mauaji ya Rais Melchior Ndadaye mwaka wa 1993.

Baadae kundi la CNDD-FDD, lilibadilishwa na kuwa chama cha kisiasa ambacho kilianza kushiriki mazungmzo ya amani mjini Arusha Tanzania mwaka wa 2000 na kuafikiana kuhusu usitishwaji wa vita.

Wakati kundi la waasi la CNDD-FDD lilipojiunga na serikali mwaka wa 2003, Ndayishimiye tayari alikuwa amepandishwa cheo cha Meja Jenerali na alihamishwa aende kuhudumu makao makuu ya jeshi la taifa.

Aliteuliwa  kuwa Waziri wa Usalama wa Ndani na Usalama wa Umma, baada ya Rais Nkurunziza kushinda uchaguzi mkuu wa mwaka 2005, na badaye kuhamishwa hadi ofisi ya Rais mwaka 2007 ambapo alihudumu kama mshauri wa kijeshi.

Wachanganuzi wa siasa za Burundi wanasema enerali Ndayishimiye ni mtu mwenye msimamo wa kadri asiyekimbilia mambo.

Wakati wa mzozo uliokumba Burundi mwaka wa 2015 kufuatia jaribio la mapinduzi, Jenerali Ndayishimiye ni miongoni mwa viongozi wachache waandamizi jeshini ambao hawakutajwa katika orodha ya wale waliohusika katika uhalifu dhidi ya binadamu na mashirika ya kimataifa.

Jenerali Evariste Ndayishimiye anachukua nchi yenye mgawanyiko mkubwa kutoka kwa kiongozi wa zamani  Nkurunziza.

Burundi inakabiliwa na migawanyiko tofauti, ikiwemo ya ukabila baina ya Watuhu na Watutsi, mgawanyiko wa kisiasa baina ya Serikali na upinzani. Jenerali Ndayishimiyeatakuwa na kibarua cha kuungana na Rwasa pamoja na wapinzani wengine kutoka vyama vya upinzani vipatavyo 40 kwa kwa ajili ya kuleta umoja na mshikamano wa Warundi wote bila kujali ukabila wala siasa kinyume na mtangulizi wake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles