27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, February 8, 2023

Contact us: [email protected]

NCCR Mageuzi yatoa neno Uchaguzi Mkuu

Saraphina Senara (UoI) -Dar es salaam

CHAMA Cha NCCR Mageuzi kimejitokea hadharani kwa mara ya kwanza tangu kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 28, kikieleza kuwa kinahitaji mazungumzo ya mezani na pamoja na viongozi wa vyama vya siasa ili kuzungumzia juu ya mchakato na mwenendo wa uchaguzi kwa kuwa hawana imani na uchaguzi huo uliogubikwa na udanganyifu.

Kauyli hiyo ilitolewa na Mwenezi wa chama hicho Taifa, Edward Simbei, alipozungumza na wanahabari ambapo alieleza kuwa wako tayari kukaa kwenye meza ya mazungumzo na vyama vyote vilivyoshiriki uchaguzi, kikiwemo chama kilichoshinda na vile vya upinzani.

Simbei ambaye alikuwa akizunguma katika ofisi za Makao Makuu ya chama hicho, Ilala Dar es Salaam jana alisema chama kinatafuta amani na usawa katika nchi ya Tanzania hivyo wameamua kuomba mazungumzo ya mezani ili kuleta amani katika yale ambayo yametokea kwenye uchaguzi ikiwa ni pamoja kutetea maslahi ya Watanzania bila kujali itikadi za vyama vyao.

“Sisi kama NCCR Mageuzi msimamo wetu na ushauri wetu kwa vyama vyote vya siasa Tanzania na wale wote wanaojiita wameshinda na wale ambao wanaitwa hawajashinda, tukae katika meza ya mazungumzo ili kufikia muafaka wa kile tulichokitengeneza kwa zaidi ya  miaka 28 kuzunguka katika kanda zote kutafuta maoni ya mfumo wa vyama vingi na kujitengenezea heshima.

 “Uchaguzi huu ulikuwa na makandokando mengi yaliyosababisha kutokuwa wa haki na msimamo wa chama ni kwamba, uchaguzi hauwezi kuwa wa haki na hii ni kutokana na sasa nchi inaelekea katika mpasuko kutokana na yale yaliyojengeka kwa vyombo vya dola na wananchi,” alisema Sembei.

Akijibu maswali ya waandishi wa habari alisema hawawezi kuungana na vyama vingine katika kutafuta haki, lakini hawahitaji kufanya hivyo kwa kuwa wanaamini amani haitokani na kufanya maandamano ila ni kukaa na kuzungumza ili kuleta maridhiano katika meza moja.

“Uchaguzi ni mchakato na kama vyote hivi vimepingwa lazima kuna kasoreo ndio maaana tunataka kurudisha hesima ya nchi yetu kwa kukaa meza moja na kama tungekua tubnataka maandamano tungetangaza hata sasa.

“Maandamano sio njia sahihi ya kuileta nchi pamoja na tusiangalie tu vyama vyetu tunatakiwa kuangalia nchi kwanza badala ya vyama vyetu maana watakaodhurika ni watanzania hivyo tunatakiwa kukaa katika meza moja ili kuleta amani katika nchi yetu,” alisema Simbei.

Pia alizungumzia kushindwa kwa mwenyekiti wa chama hicho Joseph Mbatia katika ubunge, alisema hii ni kutokana na udanganyifu uliofanywa katika uchaguzi huu ambao umepelekea kwa mwenyekiti huyo kushindwa pamoja na viongozi wengine katika chama hicho.

“Kuna watu hawana majina kama mbatiaambae anatetea uhuru na amani katika taifa hili na hao nao watasema nini kama mbatia amefanyiwa hivi hii inaonyesha wazi hata katika jimbo la kawe ambako katika kituo mgombea wetu alichopigia kura kufikia muda wa majumuisho anaonekana kuwa na kura sifuri hata aliyojipigia haikuwepo.

“Sisi tulijipanga kushionda katika majimbo ya Kinondoni, Vunjo na majimbo yote tuliyosimamisha wagombea ila kutokana na mambo yalityofanyika yamepelekea kutokea kwa mambo hayo na nchi hii inahitaji sasa kukaa chini kutafuta muafaka wake,” aliongeza Simbei.

Aidha, alivitaka vyombo vya dola kutumia hekima katika utendaji kazi ili kusaidia kuondoa chuki iliyojengeka baina yao na wananchi jamboa ambalo linaweza kuleta mpasuko katika taifa endapo hekima na busara havitatumika.

“Kama hekima na busara hazitawaongoza katika kutenda yale mnayoyafanya hii italeta maaafa na sio kila amri inaweza kutekelezwa kwa mabavu na chuki haiwezi kuisha kati ya wananchi na vyombo vya dola,” alisema Simbei.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,871FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles