26.9 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Dk Mwinyi: Nitaunda Serikali makini

Mwandishi Wetu, Zanzibar

ALIYEKUWA Mgombea wa urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk Hussein Mwinyi ameapoishwa rasmu baada ya kuibuka mshindi katika Uchagzui Mkuu wa Oktoba 28, akiahidi kuunda Serikali makini.

Akizungumza muda mfupi baada ya kuapishwa jana, Dk Mwinyi aliahidi kuunda Serikali makini itakayozingatia nidhamu na maadili ya viongozi na watumishi, utendaji kazi wenye viwango bora na kasi ya maendeleo ya kiuchumi, ikiwemo kuimarisha huduma za jamii kwa kuzitumia vyema rasilimali kwa manufaa ya wananchi wote

“Nitahakikisha pia kwamba wakati wa kipindi changu cha uongozi ninashirikiana na viongozi nitakaowateua na wananchi katika kufanikisha utekelezaji wa mipango ya maendeleo ikiwemo miongozo iliyotolewa na Ilani ya CCM ya mwaka 2020-2025, Dira ya Maendeleo ya Zanzibar ya mwaka 2020  na Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Kimataifa pamoja na ahadi walizozitoa kwa wananchi wakati wa kampeni,” alisema Dk. Mwinyi.

Alisema uchaguzi sasa umekwisha, ni wakati wa kujenga nchi na kila mwananchi afanye kazi za halali na kutambua kwamba sasa kinachohitajika ni utendaji kazi wenye viwango bora.

Dk. Mwinyi alisisitiza  Serikali atakayounda itaongozwa kwa misingi ya haki, umoja na usawa kwa wananchi wote bila kumbagua yeyote kutokana na itikadi yake, jinsia au eneo analotoka.

Alisema Wazanzibar wote ni wamoja na kila mmoja ana haki ya kunufaika na huduma kwa misingi ya usawa.

Alisisitiza atawatumikia na kuwaongoza Wazanzibar kwa misingi ya haki, uadilifu bila ubaguzi kwa yeyote kutokana na iikadi, dini, jinsia au mahali anakotoka.

Alisema anapenda kuchukua fursa hiyo kutoa shukrani kwa wazanzibar wote na pia kwa Mwenyekiti wa CCM, Rais John Magufuli ambaye alijiandaa kushiriki nao lakini alishindwa kuwepo pamoja nao kutokana an sababuz zisizoweza kuzuilika.

“Baada ya salamu hizo ninapenda kuwashukuru wananchi kwa kujitokea kwa wingi kutumia haki yenu ya kikatiba kupiga kura na kuwachagua viongozi wetu kutokana na Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.

“Kujitokeza kwenu kwa wingi kuchagua viongozi katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 28 ni kielelezo cha kukomaa kwenu kisiasa na kidemokrasia, na kutambua kuwa uchaguzi ndiyo njia sahihi ya kuwapata viongozi wa nchi yetu kwa misingi ya sheria na Katiba.

“Nawapongeza kwa kutumia vizuri haki yenu hiyo kwa kuwachagua viongozi watakaoiongoza nchi yetu katika miaka mitano ijayo wakiwemo wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na madiwani. Sote tunashukuru sana kwa heshima mliyotupa ambayo ni kielelezo cha uaminifu kwa Chama cha Mapinduzi,” alisema.

Alisema kwa upande wake,Serikali yake watahakikisha wanatumika vyema ipasavyo, kwa kuwatumikia Wazanzibar katika kuinua hali za wananchi ili ziwe bora zaidi.

Dk. Mwinyi alieleza kuwa anawapongeza pia na kwuahsukuru wananchi kwa kusherehekea ushindi kwa nidhamu na utulivu huku wakizingatia umuhimu wa kulinda amani na utulivu

Alisema hilo ni jambo kubwa kwamba uchaguzi ni mchakato wa muda tu kwa ajili ya kuwapata viongozi wa ngazi mbalimbali nchini lakini amani na utulivu ni dhana ya kudumu katika msingi wa maendeleo ya nchi.

Aliwapongeza wagombea wenzake wa nafasi ya urais ambao wameyakubali matokeo ya uchaguzi na kuyaheshimu maamuzi ya wananchi kwa kuahidi kushirikiana na serikali kuwatumikia wananchi kuijenga nchi.

Alisema atashirikiana nao kuijenga Zanzibar mpya kwa kuwa Zanzibar ni kubwa na muhimu kuliko tofauti zao za kiitikadi

Alisema amenufaika na kiufarijika kutokana na hekima busara na ushauri wa Rais aliyemaliza muda wake, Dk Ali Mohamed Shein kutokana na kuwa kiongozi anayemheshimu na alisisitiza kuwa hataacha kumlipa kwa kuendeleza jitihada zake na kufuata nyayo zake kwa kuendeleza  pale alipoishia.

Pia aliipongeza Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) kwa kufabnikisha vyema majukumu yake kama yalivyoainishwa katika Katiba ya kuandaa na kusimamia uchaguzi mkuu wa mwaka huu na hatimaye kutangaza matokeo ya urais.

USHINDI

Dk. Mwingi aliibuka mshindi katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 28 mwaka huu, hivyo anatarajiwa kuapishwa kuwa Rais wa Awamu ya Nane wa Zanzibar.

Dk Mwinyi aliibuka mshindi baada ya kutangazwa kupata ushindi wa nafasi ya urais Zanzibar kwa asilimia 76. 27 huku mpinzani wake, Maalim Seif akiwa mshindi wa pili kwa asilimia 19.87.

Baada ya kutangazwa mshindi, Dk. Mwinyi alisema amepokea ushindi huokwa mikono miwili, na kushukuru kuwa wananchi walio wengi wamemchagua yeye na chama chake cha Mapinduzi kwa miaka mitano ijayo.

“Nawashukuru kwa uvumilivu na ustahamilivu mkubwa. Niwashukuru zaidi kwa kunipigia kura za kutosheleza kuwa rasi wa Zanzibar. Nitalipa imani hii kwa utumishi uliotukuka,” Dk. Mwinyi alisema.

Dk. Mwinyi aliongeza kusema Zanzibar mpya itajengwa na Wazanzibari wote bila kujali itikadi , Zanzibar ni kubwa na muhimu kuliko tofuati zao.

“Mimi Hussein Mwinyi si bora kuliko CCM ushindi huu ni wa wana Wazanzibari wote, uchaguzi sasa umekwisha turudi kujenga Zanzibar mpya,” alisema.

Alisistiza  wafuasi wa CCM, washeherekee kwa ustaha bila kukwaza wengine kwa kuwa ushindi wasingepata pasipo kuwa na ushindani.

ILIVYOKUWA

Rais Dk. Mwinyi aliwasili uwanjani saa 4:02 asubuhi ambapo na kwenda moja kwa moja kwenye kibanda maalumu kilichokuwa kimeandaliwa.

Baada ya hapo, alipigiwa mizinga 21, kisha kukagua gwarida la vikosi vya majeshi ya ulinzi na usalama ambavyo vilitengeneza umbo alifa na omega kama ishara ya kumkaribisha rasmi kushika madaraka.

Baada ya kumaliza hatua hiyo, alikwenda kwenye jukwaa maalumu lililoandaliwa uwanjani ambapo Jaji Mkuu wa Zanzibar, Othuman Omar Makungu alimwapisha. Katika jukwaa hilo Dk. Mwinyi aliapa kwa dakika 2, na kushuhudiwa na wazee kutoka Unguja na Pemba, wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama na majaji. Kitendo hicho kilifuatiwa na sala maalumu kutoka kwa viongozi wa madhebu ya Kikristo na Kiislamu ambao wote walimuombea Mungu amzidishie heki na busara katika utawala wake.

Sherehe hizo, ziliambatana na kiapo gwaride la vikosi vya ulinzi na usalama, onyesho la ndege za kivita, kikosi maalumu cha makomandoo wa Jeshi la Ulinzi Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles