32.2 C
Dar es Salaam
Thursday, November 7, 2024

Contact us: [email protected]

Nape apata ajali, gari lapinduka

Na Hadija Omari-LINDI

MBUNGE wa Mtama, Nape Nnauye (CCM), amepata ajali ya gari katika eneo la Kijiji cha Kibutuka wilayani Liwale mkoani Lindi.

Ajali hiyo ilitokea jana akiwa njiani kutoka mkoani Mtwara kwenda Liwale kwenye mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Lindi.

Nape ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo katika gari lake alikuwa na watu wengine ambao ni Mwandishi wa Star Tv Josephin Kibiriti, Katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Nachingwea, Mohamed Chiwalo  pamoja na msaidizi wake.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Prodecina Protas, alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa Jeshi la Polisi linafanya uchunguzi ili kujua chanzo cha ajali hiyo.

MTANZANIA ilipomtafuta Nape  alisema katika ajali hiyo hakuna aliyejeruhiwa.

“Ni kweli tumepata ajali wakati tunatoka Mtama kwenda Liwale kuhudhuria mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM mkoa, lakini wote tuko salama na hapa tunasubiri gari jingine linakuja kutuchukua,” alisema Nape.

Mbunge huyo alisema kwamba hakuna majeruhi kwenye ajali hiyo na wanaendelea na safari kwenda kwenye mkutano huo.

Hii ni ajali ya pili kwa Nape ambapo Oktoba 22, mwaka 2015 wakati huo bado akiwa na nafasi ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM alipata ajali akiwa njiani kuelekea Lindi akitokea jijini Dar es Salaam.

Nape amenusurika kifo katika ajali hiyo katika eneo la Njia Nne Kilwa baada ya tairi la mbele la gari aliyokuwa akiendesha aina ya Toyota Land Cruiser kupasuka na kupinduka mara kadhaa katika eneo la Nyangao mkoani Lindi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles