Naibu Waziri anusurika kifo ajalini

0
1498

Asha Bani           |        


Naibu Waziri Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye leo Jumapili Novemba 11, amenusurika kifo baada kupata ajali eneo la Iguguno Kata ya Mkalama mkoani Singida.

Akizungumza na Mtanzania Digital Naibu waziri huyo amesema alikuwa katika ziara ya kikazi lakini anamshukuru Mungu yeye na alioambatana nao katika msafara huo wametoka salama.

“Ni kweli tumepata ajali, ilikuwa kilomita 25 kabla ya kuingia Singida nilikuwa natokea Nzega kikazi lakini namshukuru Mungu tumetoka salama wote,” amesema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here