24.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 31, 2023

Contact us: [email protected]

ILHAN OMAR: Msomali aliyetoka ukimbizini hadi ubunge Marekani

NA MARKUS MPANGALA, MITANDAONI


IDADI ya wanawake kupata nafasi ya uongozi duniani inazidi kuongezeka huku miongoni mwao wakiandika historia mpya zenye kusisimua.

Ilhan Omar (36), mwenye asili ya Somalia na Muislamu, amechaguliwa kuwa mbunge katika  Bunge la Congress nchini Marekani.

Mbunge huyo anawakilisha Jimbo la Minnesota, ambalo lina idadi kubwa ya raia wa Marekani wenye asili ya Somalia.

Kuandikwa kwa historia hiyo si tu kumetokana na dini yake bali Ilhan anakuwa raia wa kwanza mwenye asili hiyo kuchaguliwa kushika wadhifa huo mkubwa katika Taifa hilo kubwa duniani, huku akiwa na umri mdogo.

Wananchi wa Scotland waliomchagua kwa kura nyingi walifahamu maneno mawili kumhusu binti huyo. Nayo ni ‘uwezo’ na ‘umahiri’. Ilhan alionyesha uwezo mkubwa katika uchambuzi wa sera na uongozi, ndiyo maana chama chake cha Scottish National Party(SNP) kilimpeleka kwa wananchi ili aonyeshe umahiri wake zaidi.

Sambamba na mambo mengine Ilhan alionyesha uwezo mkubwa wa kuzungumza wakati wa kuomba kura. Yote hayo yanaweza kufungamanishwa kwenye neno moja, dhamira. Ushindi wake ni ishara kwamba dunia inaelekea kuwa na vijana mahiri wenye uwezo wa kuongoza.

Mwanasiasa huyo chipukizi aliingia nchini Marekani na familia yake akiwa na miaka 12, wakitokea nchini Kenya, walikokimbilia baada ya kuzuka vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Somalia mwaka 1991.

Miongoni mwa mambo yaliyosisimua ni pamoja na historia yake ya kujifunza lugha ya Kiingereza ambayo amedai kuwa aliifahamu kwa kutazama televisheni za Marekani.

Tangu aishi nchini Marekani amekuwa akijihusisha na utetezi wa haki za binadamu hususani wanawake. Utambulisho mkubwa wa mwanadada huyo ni mtindo wake wa kufunga kilemba.

Itakumbukwa kuwa Rais Donald Trump, wakati wa kuusaka Urais alionyesha kutokuwa na imani na wahamiaji wa Kisomali waishio mjini Minnesota kwa madai kuwa wanaeneza maoni ya itikadi kali.

Baada ya kuchaguliwa Ilhan ameahidi kupambana na sera za Rais Trump alizozianzisha za kuzuia watu kuingia nchini Marekani.

 

Amesema; “Mabadiliko ya kutumia siasa kama chombo cha kuleta mafanikio ndiyo yamenipa nguvu ya kuingia katika siasa na kupanua demokrasia yetu imfikie kila mtu, na kugombea kiti hiki ili kuleta sera ambazo zitasaidia watu”.

Uchaguzi huo wa katikati ya muhula umefanyika wakati Rais Trump akiwa amefikisha nusu ya muda wa uongozi wake madarakani.

Shauku ya upigaji kura imetajwa kuchochea watu wengi zaidi kushiriki zoezi hilo mwaka huu ambalo ndilo limemnufaisha Ilhan.

Katika kinyang’anyiro hicho Ilhan amemshinda kiurahisi mgombea wa chama cha Republican, Jennifer Zielinski.

Mwaka 2016 mwanadada huyo alianza kupanda ngazi kisiasa baada ya kuchaguliwa ndani ya chama cha Democratic kama mwakilishi wa wakulima na wafanyakazi katika Jimbo la Minnesota.

Katika maelezo yake Ilhan amesema kuwa ushindi huo ni muhimu kwake akiwa mwanamke tena Muislamu.

Aidha amesema ushindi wake umekuja baada ya kupambana na ugumu na ushindani dhidi ya kiongozi mwenye umri mkubwa pia ugumu wa kuwa mgombea nchini Marekani akiwa mgeni kutoka jamii ya Wasomali.

Pamoja na mambo mengine amesema nafasi yake ya ushindi ilikuwa finyu, hata hivyo alitiwa moyo kutokana na kuungwa mkono na vijana wengi.

Katika ujumbe wake amewaasa wanasiasa hasa vijana kwa kusema; ‘chochote kinawezekana’.

Ilhan amezaliwa Oktoba 4, 1981 katika Mji wa Baydhabo, jijini Mogadishu nchini Somalia. Ni mtoto wa mwisho kati ya saba kwa baba yake Nur Omar Mohamed.

Baada ya vita kuzuka nchini Somalia mwaka 1991, familia yake ilitoroka na kukimbilia katika kambi ya wakimbizi nchini Kenya.

Mwaka 2011 alijiunga katika Chuo Kikuu cha North Dakota State akichukua masomo ya Sayansi ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa.

Mwanasiasa huyo chipukizi ni mkurugenzi wa sera na miradi ya mtandao wa wanawake.

Historia hii inatukumbusha maneno ya Rais Mstaafu wa Marekani, Barrack Obama alisema kuwa mipaka baina ya nchi na nchi inavunjwa kutokana na uhusiano wa binadamu.

Tunaweza kutumia mfano wa Somalia na Marekani kupitia Ilhan na Marekani kupitia Barrack Obama.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,207FollowersFollow
567,000SubscribersSubscribe

Latest Articles