29.8 C
Dar es Salaam
Monday, October 7, 2024

Contact us: [email protected]

Naibu Waziri akagua ukarabati wa uwanja uliogharimu zaidi ya Sh. Milioni 63

Damian Masyenene, Mwanza

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza ametembelea na kukagua ukarabati wa miundo mbinu ya Uwanja wa kisasa wa Nyamagana uliopo jijini Mwanza.

Katika ukaguzi huo amejionea maboresho ya mfumo wa majitaka na majisafi, vyoo, jukwaa kuu na uzio wa ukuta vilivyogharimu zaidi ya Sh. Milioni 63.

Shonza amesema matunzo ya uwanja huo unaomilikiwa na Halmashauri ya Jiji la Mwanza hayaridhishi kwani uwanja huo haumwagiliwi kama ambavyo wataalam walielekeza na baadhi ya maeneo nje ya eneo la kuchezea yameota magugu na kuleta shida kwa Usalama wa watazamaji.

Hivyo, Naibu Waziri Shonza amewataka watendaji na viongozi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza kudumisha usafi kwenye uwanja huo.
“Suala la uendelezaji wa miundo mbinu ya michezo ni shirikishi siyo la kuiachia Serikali peke yake, tumepokea ripoti yenu lakini endeleeni kuboresha miundombinu.

“Eneo la kuchezea liko vizuri lakini bado utunzaji wake kwenye usafi hauko vizuri, mjiongeze,” amesema Shonza.

Uwanja huo ambao ni wa nyumbani kwa timu ya Alliance FC inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) kwa sasa hauna majukwaa ya kukaa watazamaji, ulijengwa na Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) kwa ushirikiano na Halmashauri ya Jiji hilo, ulikabidhiwa mwaka 2016 ukiwa umewekewa nyasi bandia huku ukigharimu Sh. Bilioni 1.8.

Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Bhiku Kotecha, ameiomba Serikali kupitia Waziri huyo isaidie kufanikisha ujenzi wa majukwaa uwanjani hapo.


Naye Ofisa Michezo wa Jiji la Mwanza, Mohamed Bitegeko amesema uwanja huo ni sehemu ya miradi 14 ya kimkakati ya halmashauri hiyo na kwamba mipango inaendelea kusukwa ili uzidi kuboreshwa na kuvutia pamoja na kuongeza mapato, ambapo kwa sasa wadau wanaohitaji kuutumia kwa mazoezi hulazimika kulipa Sh. 30,000 kwa saa mbili na Sh. 200,000 kwa siku kwa wanaofanya mabonanza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles