30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

JPM afanya mabadiliko Baraza la Mawaziri

Anna Potinus, Dar es salaam

Rais Dk. John Magufuli amefanya mabadiliko katika Baraza la Mawaziri na kuteua Mawaziri, Makatibu Wakuu na Mabalozi.

Katika uteuzi wa kwanza aliyekuwa Waziri wa Madini, Angela Kairuki ameteuliwa kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Uwekezaji.

Mabadiliko hayo yametangazwa kwa vyombo vya habari leo Januari 8, 2019 Ikulu jijini Dar Es Salaam na Katibu Mkuu kiongozi balozi, John Kijazi.

Katika mabadiliko mengine, Rais Magufuli amemteua aliyekuwa Naibu Waziri wa Madini, Dk. Dotto Biseko kuwa waziri kamili wa wizara hiyo.

“Kutokana na baadhi ya makatibu wakuu na naibu makatibu wakuu kustaafu, rais ameteua makatibu wakuu wapya wanne na naibu makatibu wakuu wawili ili kuimarisha utendaji,” amesema .

Amewataja wateuliwa hao na sehemu walizopelekwa kwenye mabano, Mhandisi Joseph Nyamuhanga (Katibu Mkuu Tamisemi), Dk. Zainabu Chaula (Katibu Mkuu Afya), Elinsi Mwakalinga (Katibu Mkuu Ujenzi), Doroth Mwaluko (Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera na Uwekezaji), Dk. Doroth Gwajima (Naibu Katibu Mkuu Tamisemi) na Dk. Francis K. Michael (Naibu Katibu Mkuu Utumishi).

“Rais amefanya uteuzi wa balozi mmoja leo ambaye alikuwa Katibu Mkuu Afya, Dk. Mpoki Ndusubisya na kituo chake cha kufanyia kazi kitatangazwa hapo baadae,” amesema balozi Kijazi.
Aidha amesema rais amefanya uamuzi wa kufungua ubalozi mpya wa Tanzania nchini Cuba na balozi atakayeteuliwa kwenda kituo hicho atatangazwa baadae, pia amefanya uteuzi wa Katibu tawala wa mkoa mmoja ambapo amemteua aliyekuwa Katibu Mkuu ofisi ya Waziri Mkuu Sera na Uratibu, Prof. Fausine Kamuzora kuwa Katibu tawala wa Mkoa wa Kagera.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles