23.6 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Nahodha Gwambina aapa Ihefu hawachomoki

Na WINFRIDA MTOI, DAR ES SALAAM

NAHODHA wa timu ya Gwambina, Jacob Massawe, amesema imetosha kwa mechi nne walizopoteza na hawatarudia makosa  katika mchezo wa kesho dhidi ya Ihefu FC utakaochezwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza.

Katika michezo minne ya Ligi Kuu Tanzania Bara iliyocheza, Gwambina ilipanda daraja msimu huu, haijapata ushindi hata mmoja na haijafunga bao lolote.

Akizungumza na MTANZANIA jana kwa simu kutoka Mwanza, Massawe, alisema kuna kitu kikubwa wamejifunza katika michezo hiyo ya mwanzo na wamekifanyia kazi kuelekea mechi ijayo.

Alisema kuwa mashabiki wa Gwambina wasife moyo na kuahidi kuanza kuwapa raha katika mchezo wa kesho na mingine inayoendelea.

“Matokeo tuliyopata katika mechi zetu zilizopita nakiri kweli si mazuri na yanatuumiza hata sisi wachezaji, lakini mashabiki wetu watambue ni hali ya mchezo wa soka.

“Mchezo ujao tutacheza nyumbani japo tutatumia uwanja wa CCM Kirumba, naahidi hiyo ndiyo itakuwa mechi ya kuturudisha katika mstari, tumekaa wachezaji na kujiuliza nini cha kufanya naamini ushindi tutapata,” alisema.

Alieleza kuwa yeye ni mzoefu wa ligi na kilichokuwa kinawakumba ni changamoto ambazo zinarekebika  kulingana na makosa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles