25.2 C
Dar es Salaam
Monday, April 22, 2024

Contact us: [email protected]

Simba kufanya ‘party’ Morogoro

Na WINFRIDA MTOI, DAR ES SALAAM

TIMU ya Simba inatarajia kufanya sherehe ya ubingwa na mashabiki wake leo mkoani Morogoro, kabla ya kuelekea jijini Dodoma kuifuata JKT Tanzania.

Wekundu wa Msimbazi hao, wanatarajia kuondoka leo asubuhi, watafikia Morogoro baada ya sherehe hizo wakiwa na kombe lao la ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, kesho alfajiri wataanza safari ya Dodoma.

Sherehe hiyo ni muendelezo wa kutoa nafasi kwa mashabiki wao kupiga picha na kombe la ubingwa kama walivyofanya sehemu nyingine.

Simba ambayo imetoka kupata ushindi mnono katika mechi zake mbili zilizopita nyumbani, itacheza na JKT Tanzania Jumapili hii kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

Mkuu wa Idara ya Habari wa klabu ya Simba, Haji Manara, alisema wameamua kupitia Morogoro kutokana na ombi la mashabiki wao, wanaotaka kufanya sherehe ya ubingwa.

 “Mashabiki waliomba timu ipitie Morogoro ili walione kombe la ubingwa, Ijumaa tutakuwa na kombe hilo Morogoro kila shabiki atapata fursa ya kuliona na Jumamosi tutakwenda Dodoma.

 “Tunakwenda kucheza mechi ya mwisho kabla ya kukutana na watani wetu Yanga tarehe 18 kwa sababu mchezo wetu wa tarehe 11 umeahirishwa kutokana na ratiba ya mchezo wa  timu ya Taifa, Taifa Stars.

“Naamini katika kipindi hicho mwalimu atakuwa amekamilisha program za maandalizi yake, tunajua matokeo yatakavyokuwa na mtani wetu ni ‘zin zala day’,” alisema.

Manara alieleza kikosi chao kipo vizuri, hawana majeruhi zaidi ya Gerson Fraga na John Bocco ambaye anaendelea vizuri na program ya mwalimu na huenda wiki ijayo akarejea uwanjani.

Manara aliwataka mashabiki wote wa Simba wa Jiji la Dodoma na wale wa mikoa ya jirani, kujitokeza uwanjani Jumapili kuipa sapoti timu yao.

“Tunaomba mashabiki wote wa Simba wajitokeze uwanjani, hata wale wa Yanga pia tunawaruhusu waje na jezi zao kutuzomea, hakuna atakayepigwa wala kufinywa, Simba ni wastaarabu na wakizomewa waona raha na  kuwaongezea mzuka wachezaji,” alisema Manara.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles