Nadya atambulisha ‘You Deserve’

0
238

Kampala, Uganda

Mwimbaji nyota wa muziki wa Injili nchini Uganda, Nadya Charisma B, amewaomba wapenzi wa muziki huo kuipokea video ya wimbo wake mpya wa You Deserve.

Akizungumza na www.mtanzania.co.tz Nadya amesema wimbo wa You Deserve umebeba ujumbe wa kumwinua na kumtukuza Mungu ambaye anastahili kupewa heshima na utukufu wote kutokana na fadhili zake kwa wanadamu.

“Ninapenda wimbo huu ukawahudumie watu wote watakaopata nafasi ya kusikiliza na kutazama video ya You Deserve ambayo tayari ipo kwenye chaneli yangu ya YouTube, hivyo naomba mashabiki wangu wa Tanzania na popote pale waendelee kunipa sapoti kwenye huduma hii,” amesema Nadya Charisma.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here