25.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Wanafunzi 634 wakatisha masomo kwa ujauzito

Na Yohana Paul, Mwanza

Jumla ya Wanafunzi wa Kike 634 kutoka wilaya saba za mkoa wa Mwanza kwa kipindi cha kuanzia Januari hadi Desemba 2020 wametajwa kushindwa kuendelea na masomo baada ya kupewa ujauzito.

Hayo yamesemwa hivi karibuni na Mkuu wa Dawati la Jinsia mkoani  Mwanza, Rebecca Kasongo alipokuwa akizungumza katika Mwendelezo wa utekelezaji wa mradi wa Sauti yangu, Haki Yangu’ wilayani Ilemela unaoratibiwa na Shirika la Kutetea Haki za Wanawake na Watoto la Kivulini. 

Alisema kwa mwaka jana pekee dawati la jinsia mkoani hapa walipokea jumla ya kesi 1,644 zinazohusisha makosa ya ukatili wa kijinsia kati yake makosa ya kubaka yakiwa 250 huku makosa ya kulawiti yakiwa 52.

Alisema, pia walipokea kesi 205 za kutorosha wanafunzi na kesi za wanafunzi kupewa mimba zilikuwa 205 huku  kwa wilaya ya Ilemela pekee kulikuwa na wanafunzi 50 wa kike waliopata mimba.

Afisa Mtendaji wa kata ya Sangabuye, John Ngoroba alisema kata za Sangabuye, Bugogwa na Kayenze ni waathirika wa kubwa wa tatizo la Mimba za Utotoni kwani kwenye kata  hizo kuna wavuvi wengi wanaishi katika mialo ambao huwarubuni wanafunzi wa kike.

Mratibu wa mradi wa ‘Sauti Yangu, Haki yangu’ kutoka Shirika la  Kivulini, Eunice Mayengela alisema  kumekuwa na changamoto kubwa ya watoto wengi kuaga wazazi wao wanaenda kujisomea usiku na hawafiki sehemu za kujisomea.

Alisema shirika lao linatekeleza mradi wa “Sauti Yangu, Haki Yangu” ulioanza mwaka 2019 na utaisha 2021 kulenga kutokomeza mimba za umri mdogo kwenye Kata za Bugogwa, Sangabuye na Kayenze ambazo zipo wilayani Ilemela.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles