32.2 C
Dar es Salaam
Thursday, February 2, 2023

Contact us: [email protected]

NACTE yafungua mafunzo ya udahili

Dk. Adolf RutayugaNA ESTHER MNYIKA, DAR ES SALAAM

BARAZA l a Taifa la Elimu ya Ufundi( NACTE), limefungua rasmi mfumo wa udahili wa pamoja (CAS)   kwa mafunzo yanayoratibiwa na baraza hilo kwa mwaka wa masomo wa 2016 /17.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Kaimu Katibu Mtendaji wa NACTE, Dk. Adolf Rutayuga alisema mfumo huo utatumika kuratibu maombi ya kujiunga na mafunzo ya Astashahada (Cheti) Stashahada (Diploma) na Shahada ya Kwanza (Bachelor Degree) .

Alisema katika mwaka wa masomo wa 2015/16, baraza liliratibu udahili wa wanafunzi katika vyuo mbalimbali kwa kozi za Astashahada na Stashahada kwa mafunzo ya afya na ualimu yaliyoidhinishwa na baraza hilo.

“Baraza pia lilishirikiana na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) kuratibu udahili wa wanafunzi wa vyuo mbalimbali kwa kozi za shahada ya kwanza kupitia mfumo wa udahili wa pamoja,”alisema Rutayuga.

Alisema mifumo hiyo miwili, imefanyika kwa ufanisi mkubwa na uliwawezesha waombaji kudahiliwa na mifumo hiyo imekuwa na mafanikio mengi.

Alisema moja ya mafanikio yaliyopatikana kwa kutumia mifumo hiyo ni kudhibiti udanganyifu wa vyeti katika udahili uliotokana na baadhi ya waombaji wanaotumia vyeti bandia .

Alisema kuwapunguzia gharama za kuomba udahili katika vyuo mbalimbali , kuiwezesha Serikali kuwa na takwimu sahihi za waombaji udahili kwa ajili ya kufanikisha mipango ya elimu ya chini na kuwawezesha waombaji udahili kujiunga na mafunzo kwa taasisi zinazotambuliwa na Serikali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,471FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles