27.1 C
Dar es Salaam
Sunday, February 5, 2023

Contact us: [email protected]

Ripoti ya wauguzi walioomba rushwa yakamilika

kigwangwalaNa Veronica Romwald, Dar es Salaam

BARAZA la Wauguzi na Wakunga Tanzania, limekamilisha ripoti ya uchunguzi dhidi ya tuhuma ya kuomba rushwa ya Sh 5,000 inayowakabili wauguzi sita wa Hospitali ya Wilaya ya Temeke mkoani Dar es Salaam.

Wauguzi hao, wanaotuhumiwa kuomba rushwa ni Hadija Salum, Beatrice Temba, Agnes Mwampashe, Elizabeth Mwilawa, Mariam Mohamed na Marion Said.

Akizungumza na MTANZANIA Dar es Salaam jana, Mwanasheria wa Baraza hilo, Isaya Nkya alisema ripoti hiyo itawasilishwa ofisi ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

“Baraza linaongozwa na sheria ya Wauguzi na Wakunga Tanzania ya mwaka 2010, tulipokea maelekezo ya naibu waziri na jana (juzi) tulikwenda hadi eneo la tukio na kuwahoji watuhumiwa hao.

“Tulilazimika kufanya uchunguzi wa haraka kama tulivyoagizwa na ikizingatiwa kwamba pale wana uhaba wa wauguzi, tumekamilisha uchunguzi na ripoti hii.

“Msajili wa Baraza ataiwasilisha wakati wowote kuanzia sasa wizarani ili aliyehusika achukuliwe hatua zaidi na wengine waendelee na majukumu yao,” alisema.

Nkya aliwataka wauguzi kuzingatia maadili ya kazi zao kama walivyofundishwa na kuacha kujihusisha na vitendo vya rushwa.

Juzi Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Khamis Kigwangala alifanya ziara ya ghafla hospitalini hapo na kuelezwa taarifa ya wauguzi kuomba rushwa ya Sh 5000 kwa mjamzito.

Kwa kuwa muuguzi aliyehusika kuomba rushwa hiyo hakujitokeza, Dk. Kigwangala aliwasimamisha kazi wauguzi hao na kuagiza baraza hilo kufanya uchunguzi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,471FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles