27.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Waziri ataka Muhimbili iongeze vitanda 100

KigwangallaNA HADIA KHAMIS, DAR ES SALAAM
NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Khamis Kigwangala ameutaka uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kuhakikisha inaongeza vitanda 100 vya wagonjwa wenye mahitaji maalumu haraka iwezekanavyo.
Agizo la Dk. Kigwangala limekuja baada ya kuelezwa kuwa hospitali hiyo ilikuwa na vitanda nane tu vya wagonjwa wenye mahitaji maalumu ambapo sasa vimeongezwa hadi kufikia 17.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, baada ya kuzindua wodi mpya ya wagonjwa wenye mahitaji maalumu, Dk. Kigwangala alisema ni aibu kwa hospitali hiyo kuwa na vitanda vinane vya wagonjwa wenye mahitaji maalumu.
“Bado Hospitali ya Taifa haijafikia viwango vya Shirika la Afya Duniani (WHO), vinavyosema kila wodi iwe na vitanda 1,500 ambapo asilimia kumi ya vitanda vya hospitali vitanda 150 viwe ICU,”alisema Dk. Kigwangala.
Alisema hivi sasa hospitali hiyo, inakabiliwa na uhaba wa vitanda 125 vya wagonjwa mahututi ikiwa ni pamoja na vifaa tiba vyote vinavyohusika kwa mgonjwa.
Ameutaka uongozi kuhakikisha inatoa mafunzo ya kuhudumia wagonjwa wenye mahitaji maalumu kwa wauguzi ili kuhakikisha mgonjwa anapata huduma inavyotakiwa.
“Kwa mujibu malengo ya WHO, mgonjwa mmoja mwenye mahitaji maalumu anatakiwa aangaliwe na wauguzi watatu na si mmoja, waliopo inawabidi wafanye kazi kubwa.
“Wauguzi hawa wanatakiwa wabadilishwe kila baada ya saa sita, kwa saa 24 lazima kuwe na zamu tatu za wauguzi ili kuweza kufikia lengo la WHO,”alisema Dk. Kigwangala.
Kutokana na hali hiyo, amemtaka Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo, Lawrence Mseru kutenga fedha kwa ajili ya mafunzo ya wauguzi, huku akiagiza Chuo cha Afya Sayansi na Tiba (MUHAS)kuhakikisha kinaanzisha kozi ya mafunzo maalumu ya wauguzi wanaotoa huduma za wagonjwa wenye mahitaji hayo.
Kwa upande wake, Museru alisema licha ya kuwa bado wapo chini ya kiwango cha WHO juhudi ya upanuzi wa wodi ya wagonjwa mahututi imefanikiwa kwa asilimia 200 na itasaidia kupunguza msongamano mkubwa wa wagonjwa hao.
Alisema hatua hiyo ya uboreshaji wa miundombinu imeweza kufikiwa kwa kutumia fedha za mfuko wa Muhimbili kwa kushirikiana na taasisi isiyokuwa ya kiserikali kutoka nchini Ujerumani.
“Hospitali ya Taifa Muhimbili imetoa Sh milioni 230 zilizotumika kwa ajili ya ukarabati wa wodi hii ikiwa ni pamoja na kutafuta ufadhili kutoka Taasisi ya Gastrenterology ya Ujerumani iliyowekeza vifaa tiba vyenye thamani ya Sh milioni 600,”alisema Profesa Mseru.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles