Mwili wa mzee Apson kuagwa leo Dar

0
1025

Tunu Nassor -Dar es salaam

MWILI wa Mkurugenzi Mkuu mstaafu wa Usalama wa Taifa, Apson Mwang’onda unatarajiwa kuagwa leo katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Petro, Dar es Salaam.

Uliwasili jana saa 8:41 mchana Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) ukitokea Afrika Kusini kwa ndege ya shirika la ndege la nchi hiyo.

Apson alifariki dunia Oktoba 7, mwaka huu nchini Afrika Kusini alikokuwa akitibiwa.

Akizungumzia ratiba ya msiba, msemaji wa familia, Emmanuel Mataluma, alisema ibada ya mazishi itaanza saa tatu katika kanisa hilo.

Alisema misa hiyo itaambatana na kuuaga mwili na kutoa salamu za rambirambi.

“Saa nane mchana mwili utapelekwa uwanja wa ndege kusafirishwa kuelekea Songwe kwa maziko,” alisema Mataluma.

Alisema mwili wa mzee Apson unatarajiwa kuzijkwa kesho katika Kijiji cha Old Vwawa, Mbozi mkoani Mbeya.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here