23.6 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Mwenge wa Uhuru kuzindua miradi sita Mbozi

Na MWANDISHI WETU-MBOZI

HALMASHAURI ya Wilaya ya Mbozi, Mkoa wa Songwe, imejipanga kukimbiza Mwenge wa Uhuru na kuwa na mikesha ya mwenge ya aina yake kutokana na maandalizi waliyoyafanya.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi, Kazimbaya Makwega, alisema maandalizi hayo ni pamoja na kutoa chakula na vinywaji bure kwa wananchi wote watakaokuwepo katika eneo la mkesha.

Kwa mujibu wa Makwega, Mwenge wa Uhuru ambao unawashwa kesho na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, utakimbizwa na kuzindua miradi mbalimbali na kuweka mawe ya msingi katika miradi sita.

“Miradi itakayozinduliwa ni pamioja na daraja lililoko katika Kijiji cha Mbozi, kuweka jiwe la msingi kwenye soko jipya la Vwawa, kufungua zahanati, kufungua kiwanda cha unga na kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa madarasa ya Shule ya Sekondari ya Kutwa ya Vwawa.

“Miradi yote hiyo itakuwa na thamani ya Shilingi bilioni 3.4,” alisema Makwega.

Kuhusu mkesha, alisema kutakuwa na burudani mbalimbali akiwamo mwanamuzi maarufu Christian Bela na wengine kwa ajili ya kupamba mkesha huo.

“Mwenge wa Uhuru ni wa wananchi na si wa viongozi, ndiyo maana tumeshirikiana nao kwa ajili ya mkesha huo ambao tuna imani utakuwa ni wa aina yake kwani kila atakayekuja, atakula na kunywa hadi asubuhi,” alisema Makwega.

Katika hatua nyingine, Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Brigedia Jenerali Mstaafu, Nicodemus Mwengela, aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye mkesha huo utakaofanyika katika viwanja vya Mlowo kesho ambako Mwenge huo wa Uhuru utawashwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles