23.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, June 6, 2023

Contact us: [email protected]

Mwanza kutoa dozi 90,000 chanjo ya UVIKO-19

NA SHEILA KATIKULA, MWANZA

Mkoa wa Mwanza unatarajia kutoa dozi 90,000 za chanjo ya UVIKO-19 ili kuwakinga wananchi wake dhidi ya madhara ya kiafya yanayotokayo ugonjwa huo.

Akitoa taarifa hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel, amesema kuwa dozi hiyo itatolewa kwa wote wenye kuridhia na wataanza na makundi maalumu ya watumishi wa afya, walio na magonjwa ya muda mrefu na watu wazima walio na umri zaidi ya miaka 50.

Gabriel amesema kuna umuhimu wa kila mmoja kupata chanjo kwani ni salama na haina madhara yoyote kiafya ambapo wananchi wanapaswa kupuuza maneno ya upotoshaji kutoka mitandaoni juu ya mitazamo hasi ya chanjo hiyo.

Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Thomas Rutachizibwa ameeleza kuwa chanjo waliyoipokea itatolewa bure hivyo ni vyema wananchi kuendelea kuhamasishana kujitokeza kupata chanjo hiyo kwani hakuna fedha yeyote itakayotozwa.

Mganga Mfawizi wa hospitali ya Rufaa Mkoa ya Sekou Toure, Bahati Peter, amesema, chanjo ya UVIKO-19 imefanyiwa uthibitisho, hivyo wanachi wasisubiri kuugua badala yake wawahi kupata kinga na kuacha kudanganyana badala yake waendelee kuchukua tahadhari kuvaa barakoa na  kunawa mikono.

Kisali Simba ni mmoja kati ya waandishi wa habari aliyejitokeza kupata chanjo  ameeleza kuwa hakuna changamoto yeyote ambayo ameipata baada ya kupata chanjo na hali inayoashiria usalama wa chanjo hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,303FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles