27.7 C
Dar es Salaam
Saturday, June 10, 2023

Contact us: [email protected]

Mume amnyonga mke akishirikiana na watoto wake

Na Allan Vicent, Tabora

MWANAMAMA Maria Kishiwa (57) mkazi wa Kitongoji cha Guluhuma Kijiji cha Isalalo kata ya Utwigu tarafa ya Puge wilayani Nzega, mkoani Tabora amekutwa amekufa mwili wake ukiwa umening’inizwa kwenye nguzo ya jiko, huku aikidaiwa waliofanya mauaji hayo ni mume  na watoto wake wawili.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani hapa, ACP Safia Jongo, amethibitisha kutokea mauaji hayo Agosti 3,mwaka huu majira ya saa nane  usiku ambapo mwili wa marehemu ulikutwa umefungwa kamba shingoni huku umening’inizwa  kwenye nguzo ya jiko.

Amebainisha kuwa chanzo cha mauaji hayo ni kuugua maradhi kwa muda mrefu ambapo mume wake akishirikiana na watoto wake  wawili waliamua kumnyonga kwa kumfunga kamba shingoni na kumning’iniza ili ionekane kajinyonga mwenyewe.

 Ameongeza kuwa eneo aliloning’inizwa walikuta kinu na kigoda ili ionekane kuwa alipanda ili kutekeleza kitendo hicho wakati ni vigumu kwa mtu kupanda hadi kuwe na msaada wa watu wengine na jambo ambalo lilileta mashaka. 

Kamanda Safia amesema kuwa marehemu alikuwa analala na mtoto wake na walipomhoji mtoto huyo alithibitisha kuwa baba alikuja usiku na watoto wake wa kiume na kumfunga kamba kabla ya kumnyonga.

Ameongeza kuwa baada ya mwili huo kufanyiwa uchunguzi wa kina na daktari ilibainika kuwa amekufa kwa kunyongwa na watuhumiwa watatu waliokamatwa walikiri kuhusika na mauaji hayo kwa sababu ya kuugua kwa muda mrefu.

Amesema watu watatu wanashikiliwa kwa tuhuma za kuhusika na mauaji hayo na uchunguzi unaendelea.

Wakati huo huo Kamanda Safia amewataka madereva wa magari na bodaboda kufanya shughuli zao kwa kuzingatia kanuni, taratibu na sheria za usalama barabarani ili kuepusha ajali huku akibainisha kuwa watafanya oparesheni kubwa ya kukagua wale wote wasiozingatia sheria za usalama.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,414FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles