MWANAPOMBE AWABARIKI ASLAY, NANDY

0
1074

NA BRIGHITER MASAKI


MKONGWE wa muziki nchini, Mwanapombe Hiyari, amewabariki wakali wa muziki nchini, Faustina Charles ‘Nandy’ na Aslay Isiaka ‘Aslay’ baada ya kufanya vizuri kwenye wimbo wake ambao wameurudia unaojulikana kwa jina la ‘Subalkheri’.

Wasanii hao wiki iliyopita walikwenda visiwani Zanzibar na kumtembelea mtumzi huyo wa muziki pamoja na familia yake. Alisema amekuwa na furaha kubwa kuwaona wasanii hao wakiutendea haki wimbo huo, hivyo amewapokea kwa mikono miwili na kuwapa baraka tele katika kazi zao.

“Sina shaka na hawa wajukuu zangu, nawaombea dua na wafike mbali zaidi kwenye maisha haya ya muziki, wamenifurahisha kwa kuwa hawajatia doa kazi yangu,” alisema Mwanapombe.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here