24 C
Dar es Salaam
Thursday, July 25, 2024

Contact us: [email protected]

KIM AWASHTUA MASHABIKI WA BLAC CHYNA

NEW YORK, MAREKANI


MASHABIKI wa mwanamitindo maarufu nchini Marekani, Blac Chyna, wameshtushwa na kitendo cha Kim Kardashian kumtumia zawadi ya siku ya wapendanao mrembo huyo.

Blac na familia ya Kardashian wamekuwa na mgogoro tangu Januari 2016, baada ya mrembo huyo kuwa kwenye uhusiano na kaka wa Kim, Rob Kardashian na kufanikiwa kupata mtoto mmoja.

Familia hiyo ilidai kuwa huyo si mrembo sahihi kwa kaka yao, hivyo walimtaka kukaa naye mbali, kitendo ambacho kiliwafanya wawe na mgogoro mkubwa, lakini cha kushangaza ni kwamba Kim amemtumia mrembo huyo zawadi ya ‘Perfume’ akidai kuwa ni kwa ajili ya wapendanao.

‘Hiki ni kipindi cha wapendanao, napenda kutumia nafasi hii kuwapa zawadi wale niwapendao, tunaochukiana, pamoja na wale wote ambao nawafikiria, hii ni kwa ajili ya siku ya wapendanao,” alisema Kim kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Hata hivyo, kitendo hicho kimewashangaza mashabiki wengi wa Blac, huku wakidai kuwa Kim anatumia njia hiyo kutangaza biashara zake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles