27.5 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

SHILOLE ASUBIRI GARI YA HARMONIZE 

NA BRIGHITER MASAKI


MSANII wa muziki na filamu nchini, Zuwena Mohammed ‘Shilole’, ameweka wazi kuwa siku za hivi karibuni anaweza kukabidhiwa gari yake kutoka kwa Harmonize baada ya kumwahidi siku ya harusi yake.

Mrembo huyo aliahidiwa gari aina ya Noah, hivyo inadaiwa kwamba gari hiyo tayari imenunuliwa na kilichobaki ni makabidhiano mbele ya vyombo vya habari.

“Ni kweli Harmonize ameniambia gari lipo tayari na kilichobaki ni kukabidhiana, mambo yakiwekwa wazi kwenye vyombo vya habari yanatakiwa kuishia huko huko, kwa kuwa watu tayari wameanza kusema kuwa nimetapeliwa, lakini ukweli ni kwamba Harmonize hashindwi kitu,” alisema Shilole.

Harmonize aliahidi gari lenye thamani ya Sh milioni 9 ili liwasaidie wawili hao katika shughuli zao za biashara.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles