23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Mwanafunzi UDSM mbaroni akituhumiwa kutoa takwimu za uongo kuhusu corona

Na DAMIAN MASYENENE -SHINYANGA

JESHI la Polisi mkoani Shinyanga linamshikilia mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Kitivo cha Kiswahili, Mariam Sanane (23) kwa tuhuma za kuchapisha na kusambaza taarifa za uongo kwenye mitandao ya kijamii kuhusu virusi vya corona.

 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, ACP Debora Magiligimba katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, alisema mwanafunzi huyo wa mwaka wa tatu alikamatwa Aprili 9 saa 2:07 usiku eneo la Mwadui, Mtaa wa Tabora kwenye machimbo ya almasi wilayani Kishapu.

Alisema mtuhumiwa alichapisha ujumbe huo kwenye mtandao wa kijamii wa WhatsApp Machi 26, mwaka huu akipotosha idadi ya visa vya corona vilivyopo nchini na idadi ya watu waliofariki kutokana na ugonjwa huo.

“Machi 26 mwaka huu askari wa kikosi kazi cha mtandao kilifanikiwa kuona ujumbe wa WhatsApp uliotumwa na mtuhumiwa unaosema ‘Mpk ss (mpaka sasa) Tanzania ina wagonjwa wapatao takribani 230 wa Covid-19 na waliofariki ni 04’.

“Mtuhumiwa amepekuliwa na kukutwa na simu iliyotumika kutuma ujumbe huo na ameshahojiwa na atafikishwa mahakamani kwa makosa ya kuchapisha na kusambaza taarifa za uongo mtandaoni na kutoa takwimu za uongo,” alisema Kamanda Debora.

Katika hatua nyingine, Kamanda Debora ametoa wito kwa wananchi kuwa makini na matumizi ya mitandao ya kijamii na kuacha kupotosha watu kwani kufanya hivyo ni kosa la jinai na hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya wale wote watakaobainika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles