23.3 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Walemavu waomba vifaa vya kujikinga na corona

NA ALLAN VICENT -Tabora

WATU wenye ulemavu mkoani Tabora wameiomba Serikali kuona haja ya kuwahimiza wataalamu wa teknolojia na ufundi kubuni au kuwatengenezea vifaa maalumu vinavyoweza kuwasaida kujikinga na virusi vya corona.

 Wakizungumza na gazeti hili jana, walisema njia za kujikinga na maambukizi ya ugonjwa huo kwa baadhi ya watu wenye ulemavu zimekuwa sio rafiki, hivyo wapo kwenye hatari ya kuambukizwa virusi hivyo.

Alisema baadhi ya vifaa vinavyohimizwa kutumika ambavyo viko katika maeneo mbalimbali mitaani haviwawezeshi baadhi yao kuvitumia, hivyo wameomba Serikali iangalie namna ya kuwasaidia ikiwemo kutengeneza vifaa vilivyo rafiki kwa kundi hilo.

 Walisema baadhi yao hawawezi kutumia vifaa vilivyopo sasa vya kunawia mikono kwa kuwa viko juu, hivyo kushindwa kunawa kutokana na hali zao.

Waliomba Serikali kuhimiza wataalamu au wadau kubuni teknolojia itakayokuwa rafiki kwao ili kuwasaidia kujikinga na maambukizi ya ugonjwa huo.

 Baadhi ya wadau wa maendeleo mkoani hapa walishauri mikakati ya mapambano ya virusi vya ugonjwa huo iende sambamba na mahitaji muhimu ya kundi la watu wenye ulemavu.

Aidha waliomba vifaa hivyo vipatikane katika maeneo yote ya kutolea huduma za jamii ili kulisaidia kundi hilo.

Mganga Mkuu wa Mkoa Tabora, Honoratha Rutatinisibwa alisema utoaji wa elimu ya kujikinga na ugonjwa huo umezingatia makundi yote.

Dk. Rutatinisibwa alifafanua kuwa ni jukumu la kila mwananchi kuhakikisha kundi la watu wenye ulemavu linalindwa na maambukizi ya virusi vya ugonjwa huo na kutanguliza utu na mahitaji yao.

 Alisisitiza umuhimu wa wadau mbalimbali wa maendeleo kuendelea kulisaidia kundi hilo katika maeneo yao ili kuliwezesha kujikinga na ugonjwa huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles