Mwamuzi kutoka Tanzania kuchezesha AFCON

0
1796

Na Johns NjoziMwamuzi wa mpira wa miguu wa kike kutoka nchini Tanzania, Jonesia Rukya, ameteuliwa kwenda kuchezesha mechi za michuano ya mataifa huru ya Africa, (AFCON) kwa wanawake nchini Ghana.

Rukya, ni miongoni mwa waamuzi 13, wa kati walioteuliwa kuchezesha mechi hizo pamoja na wasaidizi 12, kutoka katika mataifa mbalimbali barani Afrika.

Michuano ya (AFCON) ya 11 na 13 inatarajiwa kuanza kutimua vumbi nchini Ghana, Novemba, 17, hadi Desemba1.

Aidha michuano hiyo itatumika kutoa timu zitakazofuzu kushiriki kombe la Dunia la FIFA kwa wanawake mwakani nchini Ufaransa, ambapo timu tatu za juu baada ya (AFCON) kuisha ndio zitakazokuwa zimefuzu kushiriki mashindano hayo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here