32.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 5, 2024

Contact us: [email protected]

Amber Rutty, mpenzi wake wakosa dhamana warudishwa rumande

Patricia Kimelemeta, Dar es Salaam

Mcheza video za wasanii nchini, Rutfiya Abubakari maarufu Amber Rutty na mpenzi wake, Said Mtopali (21) wamerudishwa rumande kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana baada ya kusomewa mashtaka manne likiwamo la kusambaza picha za ngono kwenye mtandao wa kijamii wa Whatsap.

Awali Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliwapandisha kizimbani mcheza video huyo, Amber Ruty na mpenzi wake huyo na kuwasomea mashitaka hayo manne.

Mshtakiwa mwingine katika kesi hiyo ni James Charles maarufu James Delicious (22) anayedaiwa kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja.

Washtakiwa hao wamefikishwa mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustine Rwizile na kusomewa mashtaka yao na wakili wa serikali Mwandamizi, Nassoro Katuga aliyekuwa akisaidiana na wakili wa serikali Nguka Faraji.

Wakili Katuga alidai kuwa shtaka la kwanza linalomkabili, Amber Ruty peke yake ni kwamba kabla au Oktoba 25 mwaka huu katika maeneo tofauti ya jiji la Dar es Salaam, mshtakiwa alimruhusu mshtakiwa Mtopali kumuingilia kimwili kinyume na maumbile.

Katika shtaka la pili linamkabili mshtakiwa Mtopali, anadaiwa kufanya mapenzi kinyume na maumbile na Amber Rutty.

Aidha, mshtakiwa James Delicious anadaiwa kuchapisha na kusambaza video za kingono kupitia kompyuta kosa analodaiwa kulitenda kati au Oktoba 25, 2018 akiwa katika sehemu tofauti za jiji la Dar es Salaam.

Anadaiwa, siku hiyo alisambaza video za ngono zisizokuwa na maadili kupitia mtandao wa kijamii wa WhatsApp.

Kosa jingine la nne ni kusababisha kusambaa picha za ngono linamkabili Amber Rutty na Said Mtopali ambapo wanadaiwa kati Oktoba 25, 2018 walisababisha kusambaza picha za ngono kupitia makundi ya Whatsap, kosa ambalo wamelikana.

Kabla ya kusomwa kwa masharti ya dhamana Wakili Katuga ameieleza mahakama kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika wanasubiri taarifa za kitaalamu kutoka kwa daktari na ‘statement’ kutoka kwa mashahidi juu ya picha hizo za ngono za minato.

Hata hivyo, washtakiwa hao walikana mashtaka hayo na Hakimu Lwizile alitoa masharti ya dhamana ambapo Mahakama imewataka washtakiwa kila mmoja kuwa na wadhamini wawili waliotakikiwa kusaini bondi ya Sh Milioni 15.

Pia wadhamini wametakiwa kuwa na vitambulisho vya taifa pamoja na kuwasilisha hati zao za kusafiria, pia hawaruhusiwi kutoka nje ya Dar es Salaam bila ruhusa ya mahakama.

Hata hivyo mshtakiwa James Delicious pekee ndiye amefanikiwa kutimiza masharti ya dhamana, huku Amber Rutty na Said Mtopali wakishindwa kutimiza masharti ambapo wamerudishwa rumande hadi kesi hiyo itakaposomwa tena Novemba 12 mwaka huu.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles