29.2 C
Dar es Salaam
Friday, August 19, 2022

Mwalimu auawa, akatwa kiganja

kamanda-wa-polisi-mkoa-wa-dodoma-lazaro-mambosasa1
Lazaro Mambosasa

 

NA RAMADHAN HASSAN, DODOMA

MWALIMU wa Shule ya Sekondari ya Nkuhungu mkoani hapa, Izrael Mlowasa (40) amekutwa amefariki dunia, huku kiganja chake cha mkono wa kulia kikiwa kimekatwa.

Mwili huo umekutwa jana katika nyumba ambayo iko katika hatua ya ujenzi, eneo la Nkuhungu Chama.

Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Lazaro Mambosasa alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo alisema lilitokea Oktoba 8, mwaka huu saa 11 jioni na taarifa zilitolewa na Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Fidelis Kaishozi, baada ya wasamaria wema kumwambia kuna mwili wa mwalimu wake katika pagare (nyumba inayojengwa).

Kamanda Mambosasa alisema mara baada ya mwalimu mkuu kupewa taarifa hizo alizifikisha kwa Jeshi la Polisi ambapo walikwenda na kukuta maiti hiyo.

“Kabla ya mwili wake kuonekana akiwa ameuawa, mwalimu huyo alipotea tangu Oktoba 2, mwaka huu akiwa katika matembezi yake ya kawaida na taarifa ya kupotea kwake ilitolewa polisi.

“Marehemu alikuwa akiishi Chang’ombe Extension na inaonekana ameuawa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali kama panga kwani mwili wake umekutwa na majeraha ya aina hiyo na mkono wa kulia ukiwa umekatwa kiganja ambacho hakijaonekana,” alisema.

Kamanda Mambosasa alisema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Hata hivyo, alisema hadi sasa hakuna mtu yeyote aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo na uchunguzi unaendelea ili kuweza kubaini wahusika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,987FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles