24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Mwakyembe awataka vijana kulinda maadili

Na Beatrice Kaiza, Mtanzania Digital

WAZIRI wa zamani na Mwanasiasa Harrison Mwakyembe amewataka vijana kulinda na kuthamini Muungano, huku akiwasisitiza kuishi na kusimamia maadili ya Kitanzania ikiwa ni kuenzi maono ya Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere.

Mwakyembe akizungumza na waandishi wa habari Aprili 26, 2023 jijini Dar es Salaam katika Mdahalo wa Kitaaluma wa Chuo Cha Ustawi wa Jamii (ISW), uliyobebwa na mada isemayo ‘Maadili ya Vijana kwa Jamii’ ikiwa ni maadhimisho ya miaka 59 ya Muungano.

“Tujivunie Muungano wetu na sio kwa bahati nasibu tuwe kifua mbele, tujivunie na kuulinda Muungano ndio maana mwalimu alisema hata bila mapinduzi Tanganyika na Zanzibar ingeungana,nchi kubwa zilikiwa haziamini kama Muungano huu utadumu.

Aidha Mwakyembe aliwataka vijana wahakikishe wanapata historia sahihi ya taifa kuhusu maadili kwa lengo la kutopotoshwa na kuiga maadili kutoka nje ya nchi.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo hicho, Sophia Simba, amesema wanafunzi wa chuo hicho na maofisa ustawi wa jamii nchini wanakazi kubwa ya kutengeneza mikakati na njia sahihi ya kukabiliana na mmomonyoko wa maadili.

“Hii ni fursa kwenu watu wa ustawi wa jamii mtengeneze mikakati ya kuishawishi serikali kwa namna gani tunakabiliana na suala la mmonyoko wa maadili na kulirejesha taifa letu katika misingi bora ya maadili,” amesema Simba.

Pia, Sophia amesema kuwa jamii ifuate misingi bora ya malezi na wafanye ufuatiliaji wa kutosha wa makuzi ya watoto kwa sababu itasaidia kujenga ustawi mzuri wa taifa.

Naye Mkuu wa chuo cha ISW, Joyce Nyoni amesema Taifa likiwa na maadili mema litazidi kudumisha hata Muungano uliyopo.

Aidha mdaharo uliyofanyika chuoni hapo umelenga kuikumbusha jamii kuhusu masuala ya maadili, kwani ni jambo la muhimu katika kuhakikisha taifa linakuwa na ustawi bora.

Kwa mujibu Nyoni jamii, viongozi wa dini Tasisi za Elimu wanawajibu wa kusimamia ipasavyo suala la maadili ili kujenga kizazi bora.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles