30.2 C
Dar es Salaam
Friday, May 10, 2024

Contact us: [email protected]

Mwakinyo afungiwa kupigana, faini juu

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

KAMISHENI ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBRC), imemfungia bondia Hassan Mwakinyo  kutojihusisha na mchezo huo ndani na nje ya nchi kwa kipindi cha mwaka mmoja na kumpiga faini sh. 1milioni  kwa kitendo cha kugoma kupanda ulingoni Septemba 29,2023.

Katika pambano hilo la IBA Intercontinental,  Mwakinyo alitakiwa kupanda ulingoni , jijini Dar es Salaam kupigana na bondia Julius Indongo kutoka Nambia.

 Akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 10,2023, Katiba Mkuu wa (TPBRC), George Silas uamuzi wa kumfungia bondia huyo umetokana na kikao cha Kamati ya  Nidhamu ya misheni hiyo kilichofanyika Oktoba 5, mwaka huu.

Silas amesema kamati ilisikiliza maelezo ya pande zote mbili na vielelezo vyao lakini wakabaini  alicholalamikia  Mwakinyo hakikuwa  kwenye makubaliano ya mkataba wake na promota aliyeandaa pambano hilo, Godson Karigo.

“Mwakinyo amepewa adhabu hii kutokana na kukiuka taratibu za mkataba. Hata hivyo anaruhusiwa kukata rufaa ndani ya siku saba kuanzia leo,”amesema Silas.

Aidha  amefafanua  kuwa adhabu hiyo  pia imetolewa kama fundisho kwa kuwa Mwakinyo ni bondia mkubwa anayetakiwa awe mfano wa kuigwa na kuheshimu viongozi wake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles