26.4 C
Dar es Salaam
Tuesday, May 21, 2024

Contact us: [email protected]

Tanroads: Ushirikishwaji wa wataalamu wazawa ni nyenzo muhimu katika maendeleo

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Matumizi ya Maudhui ya ndani katika ujenzi imelezwa kuwa ni kipengele muhimu cha mkakati wa maendeleo ya uchumi wa Tanzania na kwamba iwapo hilo litazingatiwa basi itasaidia kuchochea maendeleo.

Hayo yamebainishwa hivi karibuni jijini Dar es Salaam na Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), Mohamed Besta, wakati akizungumza na Mtanzania Digital.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanroads, Mohamed Besta.

“Kwa kuweka kipaumbele katika tasnia ya ujenzi, kazi, nyenzo na utaalamu wa ndani, sekta ya ujenzi inaweza kuwa kichocheo kikuu cha ukuaji jumuishi na kuwanufaisha Watanzania kote nchini. Kwa juhudi zinazoendelea na kujitolea, sekta ya ujenzi ya Tanzania inaweza kuweka njia kwa mustakabali mzuri wa kiuchumi,” amesema Besta.

Amesema wakati wa kuweka kauli mbiu wataalamu wa ndani umefika na kwamba ni wakati wa pande zote kupitia uongozi wa ERB, CRB na PPRA ili kulichukulia suala hilo kwa umakini unaostahili.

“Ni dhahiri kwamba sera za wataalamu wa ndani, mikakati na rasilimali ni nyenzo muhimu kwa maendeleo ya kiuchumi na kukuza ukuaji – kutoa kazi na fursa kwa kampuni za ndani za ujenzi, kuwezesha uhamisho wa teknolojia, na kujenga ujuzi wa kiufundi wa ndani ambao ni muhimu kwa taifa,” amesema Besta.

Katika hatua nyingine Besta amesisitiza kwamba kutegemea kampuni za kigeni kubuni na kutengeneza vifaa si jambo endelevu, kwani utaalamu unaweza kukoma pindi ujenzi unapokamilika.

Wao wanafanya nini?

Amesema, Tanroads inasimamia mtandao wa barabara zenye urefu wa kilomita 36,760.29 ikiwa na jukumu la kuboresha barabara ikiwemo kwenye viwanja vya ndege.

Mwongozo wa Kitaifa wa kutumia wataalamu wazawa katika sekta mbalimbali uliotolewa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (2019) umebainisha kuwa sekta ya ujenzi inayopewa kipaumbele katika kuendesha ajenda ya maudhui ya ndani nchini.

Baadhi ya hatua zinazochukuliwa na serikali kukuza maudhui ya ndani katika sekta ya ujenzi na sekta nyinginezo ni pamoja na kutunga sheria na kanuni zinazohitaji makampuni ya ujenzi kuweka kipaumbele cha maudhui ya ndani katika miradi yao, kujenga uwezo wa wataalam wa ndani, kuhimiza makampuni ya ndani ya ujenzi na huduma kushindana katika miradi ya miundombinu ya ukubwa na ugumu mbalimbali, na kukuza ubia kati ya makampuni ya ndani na nje ya nchi.

Bodi ya Wakandarasi (CRB) pia ina utaratibu wa kufadhili kupitia Mfuko wa Msaada wa Wakandarasi (CAF), ambao unalenga kuwawezesha wakandarasi wa ndani kupata miradi zaidi.

Hazina hiyo ilidhamini miradi 236 yenye thamani ya jumla ya Sh bilioni 129.95 mwaka wa 2022 ili kusaidia wakandarasi kwa malipo ya awali ya jumla ya Sh bilioni 14.78, kulingana na bodi hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles