29.2 C
Dar es Salaam
Friday, May 3, 2024

Contact us: [email protected]

Mwakinyo aahidi raha Zanzibar, kuzichapa na Mzimbabwe

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

Bondia wa ngumi za kulipwa nchini, Hassan Mwakinyo, anatarajia kupanda ulingoni  kuzichapa na Mzimbabwe Enock Msambudzi, pambano litakalofanyika Januari 27, 2024 visiwani Zanzibar.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 2,2024, jijini Dar es Salaam, Mwakinyo amewahakikishia wapenzi wa masumbwi Zanzibar na Tanzania kwa ujumla kuwa watafurahi siku hiyo kutokana na maandalizi aliyofanya.

Amesema siku hiyo ataonesha burudani ya ngumi na hakuna atakayejutia kumshabikia, akitamba kuwa nyasi zitawaka moto.

Ameeleza kuwa siku zote anapocheza pambano anakuwa tayari amemsoma mpinzani wake, hivyo hatawaangusha mashabiki wake.

Aidha amesema yeye ni miongoni mwa watu waliokuwa wanapigania uhuru wa mabondia wa Zanzibar ili kupewa nafasi ya kupigana na kutoa ahadi ya kucheza pambano bure endapo itafanikiwa, hivyo fursa hiyo aliyoipata ataitumia kuwafurahisha.

“Napenda nishukuru Peaktime na watu wote lakini niwashuku Wazanzibari kwa kuwa na hamu ya kubwa ya  kuniona kutokana na mchango wangu mdogo ambao nilionyesha siku za nyuma kuwa miongoni mwa watu waliowahi kuwa msitari wa mbele kuomba Serikali ya Zanzibar kutoka fursa ya mchezo wa ‘boxing’ kama ilivyo Bara.

“Ilikuwa ni dua yangu kubwa kuwa kama siku itafanikiwa nitakuwa bondia wa kwanza mwenye CV kubwa kwenda kufanya jambo kubwa Zanzibar lakini haikuwa bahati kwani walipata nafasi wengine lakini bado Wazanzibari wameendelea kunipenda,”

Mwakinyo amesema anafanya maandalizi makubwa ili kumshikisha adabu mpinzani wake na anachowaomba waandaaji kama ikiwezekana pambano hilo liwe la ubingwa wa mkanda WBO.

Naye Mkurugenzi wa ZBC ambao ni waandaaji wa pambano hilo, Ramadhani Bukini, amesema wameshirikiana na wadau mbalimbali  baada ya kuona hawataweza kufanya wenyewe.

“Tuna furaha kubwa kufanya pambano hili na bondia mkubwa ambaye anaitangaza vizuri Tanzania na itakuwa fursa ya kiuchumi,” amesema Bukini.

Akizungumzia udhamini wao katika pambano hilo, Meneja Masoko wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ), Seif Suleimani Mohammed amesema wasingeacha jambo kubwa la michezo kama hilo liwapite bila kutoa mchango wao ukizingatia benki hiyo ni ya Serikali kwa asilimia 100.

Mohammed amesema kutokana na ukubwa wa Mwakinyo na mashabiki alionao angependekeza pambano hilo lifanyike katikati ya Uwanja wa wa Amaan.

“PBZ inadhamini Ligi Kuu ya Zanzibar lakini ni mara ya kwanza kudhamini ngumi hivyo hatutaishia hapa tutaendelea kufanya hivyo,” amesema Mohammed.

Naibu Katibu Mkuu wa Kamisheni ya Ngumi Zanzibar, Nasibu Amour amesema kazi yao kubwa ni kuhakikisha mabondia wote wanapata fursa sawa.

Kwa upande wake Balozi wa pambano hilo, James Tupatupa, amewataka wapenzi wa ngumi kukaa tayari kushuhudia burudani hiyo ya kuvutia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles