23.1 C
Dar es Salaam
Monday, September 25, 2023

Contact us: [email protected]

Mwajiri meli ya ‘Wachina wa JPM’ atua mahakamani

8

Na Kulwa Mzee, Dar es Salaam

ALIYEWAAJIRI Wachina wa ‘Samaki wa Magufuli’ walioachiwa huru, amefungua kesi Mahakama Kuu ya Tanzania akiidai Serikali zaidi ya Sh bilioni saba, kutokana na meli iliyozama na samaki waliotaifishwa.

Mdai huyo Said Mohammed alifungua kesi hiyo chini ya hati ya dharura dhidi ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), ambapo imepangwa kusikilizwa mbele ya Jaji Ama-Isario Munisi.

Mdai katika madai yake anadai Meli ya Tawariq 1yenye thamani ya Dola za Marekani 2,300,000 na fedha taslimu za kitanzania Sh 2,074,249,000 za samaki ambazo zilifanyiwa uthamini Oktoba mosi, 2009.

“Meli ya Tawariq 1 ilifanyiwa uthamini mwaka 2008 na kuonyesha kwamba thamani yake ni Dola 2,300,000 , ripoti hiyo ilitolewa na Kampuni ya Cambodia Shipping Services Ltd.

Awali mawakili waliokuwa wakiwatetea Wachina hao walidai Serikali inatakiwa kulipa Sh trilioni 1.3 ikiwa ni gharama zote, ikiwamo meli, samaki, mawakili na mabaharia wake.

Wakili hao walikuwa Kapten Ibrahim Bendera na Wakili John Mapinduzi ambaye aliwahi kudai kwamba ile haikuwa meli ya kawaida, ilikuwa ni kama kiwanda kwani ilikuwa inafanya kazi ya kuvua na kusindika.

Agosti mwaka 2014 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliwaachia huru Wachina wa ‘Samaki wa Magufuli’ na kuamuru Jamhuri iwarejeshee vitu vyao, ikiwamo meli ya Tawariq 1.

Wachina hao waliachiwa kwa mara ya pili, mara ya kwanza waliachiwa na Mahakama ya Rufaa Machi 28, 2014 , lakini walikamatwa tena na kushtakiwa upya kwa mashtaka hayo hayo yaliyofutwa.

Washtakiwa hao ni Nahodha wa Meli, Hsu Chin Tai na Wakala wa Meli ya Tawaliq 1, Zhao Hanquing, waliokuwa wakikabiliwa na mashtaka ya uvuvi haramu katika Ukanda wa Uchumi wa Tanzania.

Jamhuri iliwasilisha maombi ya kuifuta kesi hiyo mbele ya aliyekuwa Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Kisutu, Isaya Harufani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,718FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles