29 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 31, 2023

Contact us: [email protected]

Muhimbili, Aga Khan kubadilisha maumbile ya ngozi bure

Na TUNU NASSOR

-DAR ES SALAAM

HOSPITALI Aga Khan Dar es Salaam (AKHD) imeandaa kambi maalumu ya kutoa huduma ya kubadilisha na kuboresha maumbile na ngozi iliyokakamaa kutokana na ukatili majumbani, kuungua na kupata ajali kwa wanawake na watoto wa kike bure.

Sambamba na hilo watawatengenezea titi kwa waliokatwa kutokana na maradhi ya saratani kwa kutumia miili yao.

Kambi hiyo inafanywa kwa ushirikiano wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na shirika la kibinadamu la Reconstructing Women International.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Daktari Bingwa wa Upasuaji, Dk. Aidan Njau, alisema wamekuwa wakitoa huduma kwa kundi hilo kwa miaka mitano sasa kutokana na kunyanyapaliwa wanapopatwa na matatizo hayo.

Alisema kuyumba kwa kundi hilo husababisha familia kushindwa kutekeleza mipango yao ya kiuchumi na kijamii.

“Kambi hii itawasaidia wanawake kurudi katika hali zao za kawaida baada ya kurekebishiwa ngozi na maumbile yao,” alisema Dk. Njau.

Alisema wamekuwa wakiendesha kambi hiyo kila mwaka mara moja tangu 2016, lakini kutokana na mwitikio mkubwa kwa mwaka huu watafanya mara mbili.

“Pamoja na kuwasaidia wanawake, pia madaktari watapata ujuzi ambao utalisaidia taifa kuendelea kuwasaidia wanawake hao,” alisema Dk. Njau.

Aidha Dk. Njau alitoa wito kwa jamii kuwapeleka wanawake na watoto wa kike wenye majeraha hayo ili wapatiwe huduma.

“Jamii isiwafiche wanawake na watoto wenye majeraha ya kuungua, ajali na waliokatwa matiti kutokana na maradhi ya saratani, wawafikishe katika vituo vyetu vilivyopo Tanzania mzima,” alisema Dk. Njau.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,212FollowersFollow
567,000SubscribersSubscribe

Latest Articles