24.2 C
Dar es Salaam
Monday, March 27, 2023

Contact us: [email protected]

Jaji Mihayo aeleza mikakati kutangaza utalii

Na ASHA BANI

-DAR ES SALAAM

BODI ya Utalii Tanzania (TTB) imetengewa Sh bilioni 10.2 kwa mwaka 2019/20 kwa lengo la kutangaza utalii nje ya nchi na shughuli nyingine za kiutalii.

Akizungumza jana Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Jaji Thomas Mihayo, alisema kiasi hicho cha fedha kitatumika kutangaza utalii katika nchi mbalimbali ili kuongeza watalii wanaotembelea Tanzania.

“Fedha hizo mbali na matumizi ya ndani, ikiwemo mishahara ya wafanyakazi, zitatumika pia kutangaza vivutio vya utalii ndani na nje, lengo ni kufanikiwa zaidi kwa mwaka huu wa 2019/20,’’ alisema Jaji Mihayo.

Akizungumzia kuhusu kutangaza utalii nje ya nchi, alisema wamekuwa na mafanikio katika nchi mbalimbali zikiwemo Uingereza, Ufaransa na Ujerumani.

Lakini kwa sasa wanaongeza nguvu pia kwa kushirikiana na mabalozi wa nchi za China, Russia, Scandinavia, Singapore, Thailand na India.

Jaji Mihayo pia alizungumzia suala la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Julius Nyerere, Terminal III akisema ni kichocheo kikubwa cha utalii kwa kuwa watalii watatumia uwanja huo kuingia na kupata huduma inayostahili.

“Uwanja wa Ndege Terminal III utakapofunguliwa, tutakuwa na ofisi pale ambayo watalii wakifika watakuwa na fursa ya kupata huduma za kiutalii pale pale kwa kupata maelekezo, pia itakuwa imesaidia kuwapunguza matapeli ambao wamekuwa wakiwaliza watalii,’’ alisema Jaji Mihayo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,213FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles