25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, May 7, 2024

Contact us: [email protected]

Mtuhumiwa wa mauaji ya mkewe akamatwa

Na Mwandishi wetu, Kilosa

Jeshi la Polisi mkoani Morogoro linamshikilia mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Mohamedi Omari mkazi wa kijiji cha Kimamba A, wilayani Kilosa kwa tuhuma za kumuua mkewe na kumzika ndani ya chumba chao.

Mtuhumiwa huyo aliyefanya mauaji hayo Januari Mosi, mwaka huu, amekamatwa jana Machi 22, 2024.

Akizungumza tukio hilo Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Shaka Hamdu Shaka alipofika kijijini hapo, amesema kuwa baada ya kufanya mahojiano na watoto wa mama huyo aliyetambulika kwa jina la Beatrice Haiyasi wameeleza jinsi walivyopitia unyanyasaji mpaka kupelekea kukosa huduma muhimu za kielimu kutokana na kufungiwa ndani.

Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Shaka Hamdu Shaka, akiwa na viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama alipofika eneo la tukio

Ameeleza kuwa tukio hilo limebainika kutokana na mtuhumiwa huyo kudaiwa kuuza mabati ya Beatrice baada ya kumuua, ndipo kukukatokea ugomvi na mwanamke aliyekuwa akiishi naye na baadae watoto wa marehemu wakawa wanamkanya mama huyo asigombane na mtuhumiwa kwani atamuua kama alivyomuua mama yao.

“Tulipata taarifa za mama huyu kuuawa na mume wake kutoka kwa wasamaria wema hii ni baada ya kutokea ugomvi kati ya mtuhumiwa na mke wake wa sasa ndipo watoto wa marehemu wakaanza kumkanya mama huyo kuwa asigombane na mtuhumiwa huyo kwani atauawa kama alivyouawa mama yao ndipo mama huyo akatoa taarifa kwa mamlaka husika,”Shaka.

Kwa upande wao majirani wameeleza kuwa familia hiyo ilikuwa ni ngeni katika eneo hilo hawakuwa wanachangamana na wakazi wa eneo hilo kwani walikuwa ni watu wa kujifungua ndani.

Naye Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro Alex Mkama amesema tayari wamemshikilia mtuhumiwa huyo kwa uchunguzi zaidi na uchunguzi utakapokamilika atafikishwa Mahakama

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles