Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital
Mashabiki wa bondia Lutengano John kutoka Kigogo mwisho na Mburahati, wameahidi kutembea kwa miguu kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro kuhakikisha mpinzani wao Ally Mazome anapigika mapema katika pambano lililopewa jina la Hatukimbii Hatuogopi litakalofanyika siku ya Eid Pili mkoani humo.
Wakizungumzia safari hiyo, wamesema lengo la kufanya hivyo ni kwenda kumsapoti na kumhamasisha bondia wao Lutengano ili aweze kupata ushindi wa mapema dhidi ya mpinzani katika raundi ya tatu ya pambano.
“Lutengano ni bondia anaiwakilisha Kigogo na Dar es Salaam kwa ujumla. Tumuambie Ally Mazome afanye mazoezi kama anabeba viroba awe analima magimbi, mihogo, sisi tunaamini Mburahati haijawahi kutuzingua.
“Sisi hapa kwa ajili ya kumfuata Mazome, hatupandi gari, tunatembea kwa mguu,” wametamba mashabiki ambao ni Singa One na Ibada Jafar.
Kwa upande wake Lutengano amesema anajiandaa vizuri kuhakikisha snamaliza pambano hilo mapema katika raundi ya tatu ya mchezo kwa kuwapa burudani ya masumbwi mashabiki zake.