24.8 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Wanawake Segerea wataka fomu moja ya urais kwa Samia

Na Nora Damian, Mtanzania Digital

Mbunge wa Segerea, Bonnah Kamoli amewaongoza wanawake wa jimbo hilo kuchanga Sh milioni 4.5 kumwezesha Rais Samia Suluhu Hassan kuchukua fomu ya kugombea urais mwaka 2025 akisema amekuwa kielelezo cha mafanikio yaliyofikiwa nchini.

Bonnah ameanzisha harambee hiyo leo Machi 23,2024 wakati wa kongamano la wanawake aliloliandaa kutathmini mafanikio yaliyopatikana Jimbo la Segerea katika miaka mitatu ya uongozi wa Rais Samia.

Bonnah amemshukuru Rais Samia kwa kazi nzuri aliyoifanya na maendeleo aliyoyaleta katika jimbo hilo na maeneo mengine nchini.

Mbunge wa Segerea, Bonnah Kamoli (Wapili kulia), akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, fedha zilizochangwa na wanawake wa jimbo hilo kumwezesha Rais Samia Suluhu Hassan kuchukua fomu ya urais katika Uchaguzi Mkuu wa 2025.

“Tunamshukuru mheshimiwa Rais kwa sababu anafanya kazi nzuri na sisi wana Segerea ni mashahidi kwa maendeleo aliyotufanyia hasa katika sekta ya elimu, afya, miundombinu na kwa kiasi kikubwa ameitendea haki Ilani ya Uchaguzi ya CCM.

“Mama yetu amekuwa kielelezo cha mafanikio makubwa tuliyonayo leo, sisi wana – Segerea shukrani yetu kwake ni kumuunga mkono kuanzia katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu ili aendelee kutuongoza, kwahiyo tutamchangia fedha za fomu ya urais,” amesema Bonnah.

Katika zoezi hilo Bonnah aliungwa mkono na viongozi waliokuwa wamekaa meza kuu akiwemo Mwenyekiti wa UWT Ilala, Katibu, Katibu wa CCM Ilala, Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, madiwani, viongozi wa kata na matawi na baadhi ya wanawake waliohudhuria kongamano hilo ambapo zilipatikana Sh milioni 4.5.

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, ambaye alikuwa mgeni rasmi katika kongamano hilo amekabidhiwa fedha hizo na kumshukuru Bonnah na wanawake wa Jimbo la Segerea kwa hatua hiyo huku akiwataka kuendelea kumuunga mkono Rais Samia.

Makundi mbalimbali yamekuwa yakichanga fedha kumwezesha Rais Samia awanie urais katika Uchaguzi Mkuu wa 2025 ili aendelee kuiongoza Tanzania kutokana na maendeleo aliyoyafanya chini y

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles