23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Mtoto wa Kipanya akutanisha watu kuchangia damu Muhimbili

Anna Potinus, Dar es Salaam

Watu mbalimbali wamejitokeza kuchangia damu katika kitengo cha damu salama hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), leo Jumapili Septemba 1, ikiwa ni alama ya kuonesha ushirikioano wao kwa mtoto wa mtangazaji na mchoraji katuni maarufu nchini Masoud Kipanya, Malcolm Kipanya.

Hivi karibuni kupitia mtandao wake wa Instagram, Malcolm alitoa wito wa Watanzania kujitokeza hospitalini hapo kuchangia damu kwa lengo la kuwasaidia watu wenye matatizo mbalimbali.

Akizungumza na MtanzaniaDigital Malcolm amesema lengo kuu la kuanzisha kampeni hiyo ni kusaidia watu wenye matatizo mbalimbali na kwamba anatamani kuacha alama duniani kwakuwa anaamini alitumwa kuja kuwasaidia watu.

“Ninatamani sana kuwasaidia watu wenye tatizo kama langu na wale wenye matatizo mengine na kwasababu huu ni mwezi wa kuadhimisha ugonjwa unaonisumbua mimi wa Masculer Distrophy duniani, nimeona ni vyema nikahamasisha watu wengine kuja kuchangia damu ili tuweze kuwafikia watu wengi zaidi,” amesema.

Naye Afisa muhamasishaji damu MNH, Dk John Bigambalaye amesema amefurahishwa na namna watu walivyojitokeza kwa wingi kuchangia damu ambapo amewataka wahudumu wa afya wanaowadai wagonjwa fedha kabla ya kuwapatia damu kuachana na tabia hiyo mara moja kwani wanapaswa kutoa damu hiyo bure kama vile inavyochangiwa bure.

“Wale wanaopata changamoto za kutakiwa walipe fedha kabla ya kupatiwa damu wanapaswa kutoa taarifa mapema katika ofisi husika ili tuandae mazingira ya kuwakamata watu hao kwasababu kila kitu kinaenda na uthibitisho kwakuwa ukiongea tu sio rahisi kuamini,” amesema Dk Bigambalaye.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles