22 C
Dar es Salaam
Sunday, June 4, 2023

Contact us: [email protected]

MTOTO WA KHLOE AFIKISHA MASHABIKI 120,000

OHIO, MAREKANI


MTOTO wa mwanamitindo maarufu nchini Marekani, Khloe Kardashian, True Thompson, amefikisha jumla ya mashabiki 120,000 kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Mtoto huyo wa kike ambaye ana siku sita tangu kuzaliwa kwake, ametikisa kwenye mtandao huo wa kijamii ikiwa hata picha yake haijawekwa wazi hadi sasa.

Wazazi wa mtoto huyo, Khloe Kardashian na Tristan Thompson, waliamua kumfungulia akaunti hiyo ili kuona uwezekano wa kuja kuwa staa.

Hata hivyo, inadaiwa tangu kufunguliwa kwa akaunti hiyo, bado wazazi hao hawajaposti kitu chochote, lakini mashabiki wanazidi kumiminika.

Juzi familia ya Kardashia iliwasili mjini Ohio kwa ajili ya kumtembelea ndugu yao, Khloe na kumpa hongera kwa kujifungua salama.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,284FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles