29.3 C
Dar es Salaam
Thursday, June 1, 2023

Contact us: [email protected]

BEN POL, EBITOKE WAFANYA KWELI

NA JESSCA NANGAWE


BAADA ya ukaribu wao kuendelea kudumu huku mashabiki wengine wakiamini ni wapenzi, wasanii Benard Pol na Anna Exavery ‘Ebitoke’ wameamua kutoa wimbo wa pamoja unaojulikana kwa jina la ‘Natuliza Boli’.

Ben Pol ameamua kumshirikisha msanii huyo baada ya kuwaahidi mashabiki zake kuwa moja ya mambo atakayoyafanya kwa mwaka huu ni kumshirikisha msanii huyo wa vichekesho katika kazi zake.

Mbali na kazi hiyo, Ben Pol ameweka wazi kuwa kuna kazi nyingine nyingi zinakuja huku akiwa na mrembo huyo.

“Kufanya kazi na Ebitoke ni moja ya ndoto zangu, tulijiwekea nia hiyo ya kufanya kazi pamoja, Ebitokea ni mshikaji wangu wa karibu sana na tutaendelea kushirikiana katika kazi zetu kila itakapohitajika,” alisema Ben Pol.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,225FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles