Mtoto wa John Legend hapendi kupigwa picha

0
847

New York, Marekani

MTOTO wa staa wa muziki nchini Marekani, John Legend, anayejulikana kwa jina la Luna, anadaiwa kuwa kitu kikubwa ambacho anakichukia ni kupigwa picha.

Luna mwenye umri wa miaka mitatu, muda mwingi amekuwa akifuatana na mama yake Chrissy Teigen mara kwa mara kwenye vipindi vyake ya runinga, hivyo muda mwingi amekuwa akificha sura yake wakati wa kupigwa picha.

Chrissy mwenye umri wa miaka 34, aliuambia mtandao wa People, na kudai amekuwa akimshangaa mwanawe jinsi anavyochukia kupigwa picha.

“Ukweli ni kwamba mwanangu Luna anachukia sana kupigwa picha, hapendi kukutana na waandishi wa habari ambao wamebeba kamera, lakini anapenda kuangalia picha kwenye ukurasa wangu wa Instagram,” alisema mama wa mtoto huyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here